Je unafahamu umuhimu wa apple?

Imesomwa mara 1212

Wanasema kula apple moja kwa siku huondoa umuhimu wa kumuona daktari. Je unafahamu kwanini?

Apple ni tunda linaloleta afya kwa binadamu. Cha muhimu zaidi ni kuwa, apple husaidia kurekebisha kiwango cha mafuta kwenye damu na kufanya mishipa ya damu kupitisha damu kirahisi. Hii huzuia magonjwa tofauti yakiwemo yale ya moyo. Uwepo wa mafuta mengi kwenye mishipa ya damu ni hatarishi kwa afya yako na afya ya moyo wako pia.

Kula apple, boresha afya na maisha yako.

Toa maoni yako