Sababu 12 za kutumia Korianda kutibu magonjwa

Imesomwa mara 1839

Mbegu za korianda ( giligilani) zinatumika kama kiungo cha chakula pia kinatumika kama dawa kwenye jamii za nchi za Mashariki ya kati na Asia. Kiungo hiki hutumika kwenye mapishi ili kukifanya chakula kiwe na ladha tamu na harufu nzuri.

Korianda ni chanzo kizuri cha virutubisho kama madini ya potassium, madini chuma, Vitamin A, K and C, Folic acid, Magnessium na Calcium.

Jinsi ya kuandaa

Menya maganda, bandika kikaango jikoni na acha kipate moto sana. Weka mbegu za korianda, punguza moto, zipashe kwa moto wa wastani huku ukikoroga mara kwa mara. Hii itakufanya upate matokeo mazuri sana.

Mbegu zitakua tayari endapo zitaanza kutoa harufu nzuri. Epue na ache zipoe. Hapo unaweza kusaga zikawa unga au unaweza kutumia kama zilivyo.

Faida za korianda

Baadhi ya faida za Korianda ni :

1. Kusaidia mmeng'enyo wa chakula.

Mbegu za korianda na majani yake zinasaidia kwenye utendaji kazi wa ini na pia kuufanya mwili uzalishe vimeng’enyo vinayotumika kwenye kusaga chakula.

Ni kiungo kizuri kutumia kama umevimbiwa. Ili kupunguza kuvimbiwa unaweza kufanya hivi :

  • Loweka mbegu za korianda kwenye glass ya maji kwa siku nzima kisha chuja na kunywa maji kabla hujala kitu chochote.

2. Kutibu vidonda vya tumbo

Korianda ni chanzo kizuri cha Folic acid, Vitamin C, Vitamin A na Beta carotene. Mbegu za korianda na majani yake zina asilimia 30 ya Vitamin C iliyopendekezwa kwa siku.

Vitamin C inasaidia kukinga mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali pia kusaidia kuponyesha vidonda. Uwepo wa kiwango kikubwa cha Vitamin C hukupa uhakika wa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo, mafua, midomo kuchubuka.

3. Kinga ya kisukari

Matumizi ya korianda yanahusishwa zaidi na kupungua kwa maradhi ya kisukari mwilini. Hii ni kutokana na kuwa korianda huchochea uzalishaji wa insulin ambayo hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

Vilevile, korianda hupunguza kiwango cha lehemu (cholesterol) mbaya na kuboresha kiwango cha lehemu nzuri kwenye damu. Watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na wale wenye uwingi wa lehemu mbaya wanashauriwa kunywa maji ya korianda kila siku ili kupunguza maradhi haya.

4. Kuzuia madhara ya Salmonella

Salmonella ni bakteria anayepatikana zaidi kwenye maji, hasa yasiyo salama, na vyakula anayesababisha magonjwa kama typhoid, kuhara, na homa ya matumbo. Ulaji wa korianda mara kwa mara wa umeonekana kusuidia kupunguza madhara ya bakteria hawa mwilini.

5. Kukinga Anaemia

Korianda zina kiwango kikubwa cha madini ya chuma yanayosaidia kuongeza kiwango cha damu.Ni vizuri kutumia korianda na majani yake kwenye milo yetu ya kila siku.

6. Kutoa uchafu na sumu mwilini (Detoxification)

Kuna baadhi ya vyakula vina mkusanyiko wa kiwango kidogo za chembechembe zenye sumu kama vile mercury, arsenic, mercury na aluminium. Ulaji wa hivi vyakula hulimbikiza hizi sumu kwenye damu na huweza kuleta magonjwa kama Alzheimer, ambao humfanya mgonjwa apoteze kumbukumbu, upofu na mishipa ya damu kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha. Korianda husaidia kufyonza sumu zilizomo kwenye damu na kuzitoa bila kuleta madhara mwilini.

7. Kuzuia magonjwa ya macho

Korianda ni moja ya tiba ya kiwambi ute (conjunctivitis) kwa kupunguza wekundu, kuwasha na kuvimba macho.

8. Husaidia wanawake kwenye hedhi

Kwa wanawake wanaokabiliwa na matatizo ya hedhi korianda ni suluhisho muafaka kwenye vyakula vyao vya kila siku.
Kwa wanawake ambao mzunguko wao wa hedhi hauheleweki wanashauriwa kuchemsha korianda iliyochanganwya na maji na sukari. Mchanganyiko huu unywewe wakati bado wa moto, mara tatu kwa siku.

9. Kutibu magonjwa ya ngozi

Korianda inatibu magonjwa mbalimbali ya ngozi kama ukurutu, vipele, harara na ngozi kuvimba.
Changanya korianda ya unga, maji na asali. Koroga vizuri iwe nzito kisha paka sehemu yenye tatizo.

10. Kutibu chunusi

Korianda hutumika kutibu chunusi na madoa doa kwenye ngozi. Changanya korianda, asali na manjano ( bizari), kisha paka kwenye sehemu zilizoathirika. Kwa ngozi yenye mafuta ongeza multani mitti. Kama ngozi ni kavu osha na maji baridi kabla ya kupaka.

11. Kuboresha afya ya nywele

Changanya korianda ya unga pamoja na mafuta ya nywele kisha paka kwenye ngozi mara 2 kwa wiki Hii inasaidia nywele ziache kukatika na kuzifanya imara na zenye afya kuanzia kwenye mizizi.

12. Kutibu vidonda mdomoni

Vidonda vya mdomoni mara nyingi vinakua vyeupe vimezungukwa na wekundu. Changanya korianda na maji. Chuja maji na tumia kusukutua mdomoni.

Toa maoni yako