Jinsi ya kuzuia kitunguu kukutoa machozi

Imesomwa mara 791

Je huwa unapata shida wakati wa kumenya na kukata vitunguu kwa kutoa machozi?

Hii ni njia rahisi ya kuepukana na adha ya kulia wakati wa kukata kitunguu. Kata kitunguu ndani ya maji, hii itafanya gesi yote inayotoka kwenye vitunguu kunyonywa na maji. Hutopata madhara ya kutoa machozi. 

Ni muhimu pia kuzingatia, mara baada ya kumaliza kukata vitunguu, osha vizuri na kausha kabla ya kupika. Hii itapunguza muda wa vitunguu kuiva na kurusha mafuta wakati wa mapishi. 

Toa maoni yako