Bagia za dengu

Bagia za dengu. Kitafunwa maarufu cha kila siku. Unaweza kuongeza viungo ili kuvipa ladha zaidi.

Mahitaji

 • Ndegu kikombe 1
 • Curry powder nusu kijiko cha chai
 • Vitunguu 2
 • Kitunguu saumu  nusu kijiko cha chai
 • Pilipili 1
 • Parsley kijiko 1 cha chai
 • Maji nusu kikombe
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Mafuta
 • Pilipili hoho robo kikombe
 • Bizari nyembamba nusu kijiko cha chai
 • Baking powder kijiko 1 cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kula bagia hizi muda wowote, lakini muua kabisa kula asubuhi wakati wa chai.

 • Andaa vitunguu maji, pilipili na parsley. Kata vipande vidogo
 • Kwenye bakuli, weka unga wa dengu kisha weka currypowder, vitunguu maji, kitunguu saumu, pilipili, parsley, baking powder, bizari nyembamba, pilipili hoho na chumvi. Changanya vizuri ili viugo vichanganyikane.
 • Ongeza maji kidogo kwa wakati huku ukichanganya hadi mchanganyiko uwe mzito, uwe kama mchanganyiko wa keki. Acha mchanganyiko pembeni kwa dakika chache.
 • Bandika kikaango jikoni na weka mafuta ya kula. Mafuta yakishachemka chota mchanganyiko kwa kijiko kisha weka kwenye mafuta. Usirundike sana unga ili kuzuia bagia zisishikane.
 • Bagia zikianza kuiva na kuanza kubadilika rangi upande mmoja geuza ili zisibabuke. Zikiiva vizuri epua weka pembeni. Weka mahali zichuje mafuta.

misosi-dengu-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Kachori tamu zenye giligilani
dakika 20
Walaji: 6

Keki tamu ya mtindi na vanilla
dakika 50
Walaji: 8

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.