Bagia za kitunguu (Onion Rings)

Umeshakula bagia tofauti, je umeshawahi kula bagia yenye vitunguu? Hizi ni bagia tamu, rahisi kuandaa na unaweza kuandaa na kula muda wowote. Ni kitafunwa kizuri kwa wale wanaoenda picnic au kwa watoto wanaoenda shule.

Mahitaji

 • Kitunguu 1 kikubwa
 • Unga wa ngano ¼  kilo
 • Kiini cha yai 1 (teganisha ute na kiini)
 • Chumvi ½ kijiko kidogo
 • Maziwa ¼ kikombe
 • Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive oil)
 • Mtindi (Sour cream) na mayonnaise (Sauce ya kula na bagia za vitunguu)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza na kupunguza viungo kutokana na unavyopendelea.

 • Menya na kata vitunguu kwenye umbo la duara na viwe na umbo la duara (ziwe kama pete) ila visiwe vipana sana maana havitoiva vizuri.

Kwa unga wa ngano:

 • Pasua yai kisha tenganisha ute na kiini.
 • Changanya unga, kiini cha yai, maziwa, mafuta ya kula na chumvi. Koroga pamoja hadi vichanganyike vizuri na uwe laini.
 • Changanya kidogo kidogo ute wa yai kwenye mchanganyiko huku unakoroga.
 • Chovya vitunguu katika mchanganyiko wa unga. Hakikisha vimezama kabisa, acha vikae kwa muda kiasi ili unga upate kugandia kwenye vitunguu. Unaweza pia kuweka chenga za mkate mkavu (breadcumbs) ili kuipa umbo pana zaidi.
 • Bandika mafuta ya kula jikoni (nimetumia olive oil), acha yapate moto vizuri san kisha weka vitunguu vilivyopakwa ngano na kaanga kwa muda wa dakika 5 hadi 7 ili kiive vizuri kwa nje na ndani kiwe laini. Hakikisha mafuta yapo ya kutosha ili kila kitu kizame kwenye mafuta. 

Unaweza pia kupika hizi bagia kwa kutumia oven, kwa wale wasiopenda mafuta mengi. Ili kuoka kwenye oven, ziweke kwenye jokofu kwanza ili zigande na kuwa ngumu kiasi cha kuiva vizuri kwenye oven bila kuharibika.

 • Toa vitunguu jikoni, weka kwenye karatasi laini (paper towel) ili kunyonya mafuta na kuziacha kavu. Rudia zoezi hili kwa vitunguu vilivyobaki hadi viishe.
 • Unaweza kula haya maandazi ya kitunguu kwa chai, kama mojawapo ya sehemu ya chakula kikuu au kitafunwa cha kusindikiza kinywaji baridi. Jirambe na maandazi haya matamu ya kitunguu ila usisahau kuchanganya na sauce unayopenda - mayonnaise, ketchup, mtindi n.k.

misosi-onion-rings-mail-2


MAPISHI YAPENDWAYO

Supu ya ulimi wa ng'ombe
dakika 40
Walaji: 1

Kuku wa kukaanga wa ndimu
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.