Bagia za kunde

Bagia za kunde ni nzuri na tamu,unaweza kula na familia yako wakati wowote na mkafurahi.

Mahitaji

 • Kunde zisizo na maganda nusu kilo
 • Vitunguu maji 3
 • Vitunguu saumu 2
 • Chumvi
 • Mafuta
 • Pilipili 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Weka maji kwenye sufuria, beseni au chombo chochote.
 • Weka kunde kwenye hayo maji uziloweke, mimi huwa napendelea kuziloweka usiku mzima ili zilainike vizuri.
 • Andaa viungo, kata vitunguu maji vipande vidogo sana, vitunguu saumu menya weka kwenye chombo na pilipili ikatekate.
 • Chukua blenda, toa kunde kwenye maji, ziweke kwenye blenda.
 • Weka vitunguu maji, vitunguu saumu, pilipili na chumvi humo ulipoweka kunde
 • Ongeza maji kidogo sana,upate urahisi wa kusaga. Hakikisha unaposaga kunde zimelainika na viungo ulivyoweka vimesagika vizuri.
 • Hakikisha pia mchanganyiko hauwi mwepesi, bandika sufuri jikoni, weka mafuta yakipata moto, chukua kijiko chota ule mchanganyiko, weka kwenye mafuta.
 • Usigeuze mpaka uone chini imeiva vizuri geuza upande wa pilipili, ukiona imeiva epua, chuja mafuta hapo ni tayari kuliwa.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kashata za nazi
dakika 12
Walaji: 5

Pizza yenye sausage topping
dakika 15
Walaji: 1

Togwa
dakika 30
Walaji: 4

sweet and sour chicken
dakika 25
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.