Banana muffins

Banana muffins ni nzuri na rahisi kuoka mana hazichukui muda. Pia ni tamu na mtaenjoy na familia na marafiki.

Mahitaji

 • Unga vikombe 2
 • Baking soda kijiko 1 cha chai
 • Baking powder kijiko 1 cha chai
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Ndizi 3 kubwa zilizoiva vizuri
 • Buttermilk vijiko 3 vya chakula
 • Maziwa vijiko 3 vya chakula
 • Yai 1
 • Vanila robo kijiko cha chai
 • Nutmeg nusu kijiko cha chai 
 • Sukari robo tabu ya kikombe
 • Mdalasini robo kijiko cha chai
 • Butter vijiko 5 vya chakula pia unaweza kutumia mafuta ya kawaida au blueband

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Pasha oven nyuzi joto 190°C, kama hautumii zile karatasi za cupcakes paka mafuta zile pan zenye vikombe vya kuokea.
 • Chukua bakuli, weka unga, baking soda, baking powder, chumvi, nutneg kisha changanya vizuri sana.
 • Yeyusha butter. Menya ndizi ikate vipande vidogo vidogo,ongeza sukari, maziwa, buttermilk na yai kisha anza kuziponda. 
 • Ongeza butter na changanya vizuri.
 • Chukua mchanganyiko wenye ndizi changanya kwenye ule wenye unga, kisha anza kukoroga uchanganyikane wote kwa pamoja vizuri.
 • Ukiwa tayari, chukua mfuko msafi weka ule mchanganyiko kwenye mfuko,kata pembeni kwa mkasi kisha anza kubinya mchanganyiko uingie kwenye vyombo vya kuokea au kama una mashine tumia.
 • Weka pembeni, kisha chukua bakuli lingine weka sukari vijiko 2 vya chai, unga vijiko 2 vya chakula, mdalasini na butter changanya vizuri.
 • Kisha weka mchanganyiko huo juu ya mchanganyiko ule ulioweka kwenye vyombo vya kuokea, oka kwa dakika 20.
 • Epua anza kujiramba na marafiki.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa kuoka na ndizi mzuzu
dakika 60
Walaji: 4

Salad yenye nyama ya kuoka
dakika 45
Walaji: 3

Kashata za nazi
dakika 12
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.