Bata wa mchuzi wenye Bizari

Nyama ya bata ni tamu, hasa ikiandaliwa vizuri. Si kila siku tuna andaa bata, lakini ukitaka kuandaa bata vizuri kwa muda mfupi, hili ndio pishi la kuangalia. Hili pishi ni rahisi lenye matokeo mazuri.

Mahitaji

 • Bata mzima 1
 • Bizari vijiko 2 vya chakula
 • Pilipili manga ya unga kijiko 1 cha chakula
 • Karoti 1
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu cha unga kijiko 1 kidogo
 • Tangawizi 1
 • Nyanya 1 kubwa
 • Chumvi
 • Vinegar nusu kikombe kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kula bata, na huyu bata ni mtamu haswa. Unachotakiwa ni kujaribu tu. Kazi kwako, maana maelezo rahisi haya hapa:

misosi_nyama_bata

 • Andaa bata, kata vipande, osha vizuri.
 • Kwenye sufuria, weka bata, chumvi, kitunguu saumu, tangawizi na vinegar. Bandika jikoni, usiongeze maji. Maji ya bata yakikauka ongeza maji kikombe kikubwa 1, acha achemke tena.  

Bata anachelewa kuiva, siyo kama kuku wa kisasa, hivyo kuwa makini kuhakikisha bata ameiva vizuri ili kupata matokeo mazuri.

 • Kata kitunguu maji na karoti  kisha weka kwenye sufuria yenye bata. Koroga pamoja vizuri, takribani dakika 5, kisha weka nyanya. Funika, acha nyanya iive vizuri.
 • Weka bizari na pilipili manga, koroga pamoja. Ongeza maji kidogo. Funika mpaka maji yakauke kisha epua.
 • Tenga na ujirambe

misosi_bata_mtamu_main


MAPISHI YAPENDWAYO

Mishikaki mitamu yenye papai
dakika 30
Walaji: 6

Kababs za kuku na mayai
dakika 20
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.