Beef masala

Beef masala ni kitoweo kizuri sana, unachoweza kula na aina yoyote ya chakula na ukafurahi.

Mahitaji

 • Nyama kilo 1
 • Vitunguu maji 2
 • Nyanya 5
 • Vitunguu saumu
 • Tangawizi
 • Pilipili manga vijiko 2 vya chai
 • Pilipili iliyosagwa vijiko 3
 • Garam masala kijiko 1
 • Bizari nusu kijiko
 • Butter
 • Majani ya rosemary

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chemsha nyama, tia chumvi, bizari na pilipili kidogo.
 • Bandika sufuria jikoni weka butter, tangawizi, kitunguu saumu, majani ya rosemary na pilipili manga.
 • Ongeza vitunguu koroga mpaka viwe kahawia, weka garam masala koroga kwa dakika kumi Kisha weka bizari.
 • Weka nyanya koroga vizuri, weka nyama koroga mpaka uhakikishe imeingia viungo.
 • Ongeza maji kidogo acha ichemke mpaka maji yakauke. 
 • Hapo itakua tayari. Ruksa kujiramba

MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wa kukaanga
dakika 15
Walaji: 4

Viazi vya mayai na kamba
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.