Beef Masala

Uzuri wa vyakula shurti uwe na viungo mbadala wa kukiandaa. Nyama inaweza kupikwa mapishi mengi sana, hili la masala likiwa mojawapo. Hii mboga ina mchanganyiko wa viungo tofauti vinavyoleta harufu tamu, ladha bomba na mvuto wa chakula. Ni mboga unayoweza kula na chakula chochote kile, na wakati wowote ule.

Mahitaji

 • Nyama kilo 1
 • Vitunguu maji 2
 • Nyanya 5, zilizoiva vizuri
 • Vitunguu saumu 2
 • Tangawizi 1
 • Pilipili manga vijiko 2 vya chai
 • Pilipili iliyosagwa vijiko 3
 • Garam masala kijiko 1
 • Bizari ½ kijiko
 • Siagi (Butter)
 • Majani ya rosemary

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza na kupunguza mahitaji kutokana na upendavyo.

 • Andaa nyama – kata kisha osha. Weka kwenye sufuria safi, weka chumvi, bizari na pilipili kidogo. Bandika jikoni acha ichemke vizuri. Hakikisha huongezi maji, acha nyama ichuje maji yaliyomo ndani yake. Nyama ikishaiva vizuri itoe na hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria tofauti jikoni, weka siagi (butter), tangawizi, kitunguu saumu, majani ya rosemary na pilipili manga. Acha viive kwa dakika 2. Weka vitunguu maji, koroga mpaka viwe rangi ya kahawia. Weka garam masala kisha koroga kwa dakika 6 hadi 8.
 • Weka bizari, koroga pamoja. Baada ya dakika chache weka nyanya, koroga pamoja.
 •  Nyama ikishaiva, changanya kwenye sufuria yenye viungo. Koroga pamoja hadi nyama iingie viungo vizuri.
 • Ongeza maji kidogo kwenye nyama kisha acha ichemke mpaka maji yakauke.

Unaweza kuweka kiminika tofauti kulingana na upendeleo wako, mfano tui la nazi, maji ya chungwa au yeyote unayotaka kuleta ladha nzuri kwenye chakula. Upishi ni ubunifu tu.  

 • Maji yakikauka, nyama itakuwa imeiva vizuri. Andaa chakula na ujirambe.

beef_curry-misosi-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Omelette za pilipili hoho
dakika 5
Walaji: 1

Kuku wa mboga za majani
dakika 15
Walaji: 2

Ndizi mzuzu na sausage
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.