Beef Rendang

Beef rendang ni chakula cha kiindonesia kinachotayarishwa kwa kupika nyama yenye tui la nazi kwenye moto mdogo kwa muda mrefu hadi mchuzi wote unapokauka vizuri na kubakisha rojo ya mchuzi mzito.

Mahitaji

 • Nyama iliyochemshwa kilo 1
 • Nyanya 4
 • Nyanya paste kijiko 1 cha chai
 • Pilipili kavu 2
 • Kitunguu saumu 1
 • Tangawizi  kijiko1 cha chai
 • Mafuta vijiko 2 vya chai
 • Limao 1
 • Chumvi kiasi
 • Tui la nazi kikombe 1
 • Sukari kiasi
 • Curry powder nusu kijiko cha chai
 • Giligilani nusu kijiko cha chai

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kutokana na matakwa yako.

mis-b

 • Kwenye kinu, weka pilipili, tangawizi, kitunguu saumu, curry powder na giligilani kisha twanga mpaka vilainike. Hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta. Mafuta yakichemka weka viungo vilivyotwanga. Punguza moto kisha pika kwa dakika 10. Viungo vikianza kunukia weka nyanya. Koroga. Pika hadi ziive, weka nyanya paste. Pika kwa dakika 5, kuwa makini usiunguze. Geuza geuza taratibu ili kuchanganya pamoja.
 • Weka nyama kwenye sauce ya nyanya kisha weka tui la nazi na chumvi. Koroga hadi tui lichemke. Kisha acha ichemke kwa dakika 40 kwenye moto mdogo sana. Hakikisha nyama imelainika vizuri.
 • Weka sukari, ongeza moto kisha pika kwa dakika chache mpaka sauce iwe nzito kisha epua.
 • Unaweza kula nyama hii na wali, ugali, maandazi, mihogo, viazi au vyakula vingine vyote unavyopendelea. Jirambe

beef-m


MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa kuku na mayai yake
dakika 40
Walaji: 4

Viazi vya mboga mboga
dakika 18
Walaji: 2

Salad ya mahindi na samaki
dakika 0
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.