Biryani ya nyama

Biryan ni mchanganyiko wa vyakula kama mchele,nyama,mboga za majani na viungo tofauti vya chakula. chakula hiki asili yake ni India na ni kitamu sana. Biryani inataka kufanana na pilau

Mahitaji

 • Mchele wa Basmati kilogram 1
 • Nyama kilogram 1
 • Tangawizi
 • Kitunguu saumu
 • Binzari
 • Pilipili manga
 • Vitunguu maji nusu kilogram
 • Nyanya nusu kilogram
 • Mafuta 250gram au Samli 240gram
 • Pilipili nyekundu kijiko 1 cha chai
 • Giligiliani vijiko 3 vya chai
 • Korosho 50gram
 • Mintleaves 30gram
 • Chumvi
 • Hiliki

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Bandika nyama jikoni weka tangawizi, kitunguu saumu, binzari, pilipili manga na chumvi, hakikisha nyama imeiva ila iwe na mchuzi.
 • Epua weka pembeni .
 • Chukua vitunguu maji vikate mviringo na nyanya zikate vipande vidogo vidogo, hakikisha nyanya ni nyekundu.
 • Bandika mafuta jikoni kwenye sufuria kaanga ile nyama mpaka iwe ya kahawia kisha iepue na uichuje mafuta na weka pembeni.
 • Weka vitunguu baadhi kwenye yale mafuta vikaangempaka viize weka binzari, unga wa pilipili nyekundu, giligiliani, mbegu za hiriki na nusu mbegu za pilipili manga.
 • Changanya vizuri viungo, hapo utapata mchanganyiko mzuri kisha mimina ule mchuzi wa nyama.
 • Weka nyanya kwenye ule mchanganyiko, pika mpaka mchuzi wote ukauke yaonekane mafuta.
 • Weka nyama alafu weka chumvi, koroga vizuri kwa dakika tano kisha epua.
 • Bandika sufuria nyingine weka mafuta na vitunguu, weka majani ya giligiliani, majani ya mint na korosha, funika kwa dakika 15 kisha weka wali wako.
 • Ongeza vikombe vitano vya maji na chumvi kisha funika chakula.
 • Punguza moto mpaka maji yakauke, chukua ule mchanganyiko wenye nyama mwagia nusu tu juu ya wali acha uive.
 • Baada ya dk kumi funua chakula geuza na uhakika kitakua tayari kwa kuliwa.

MAPISHI YAPENDWAYO

Salad yenye sausage
dakika 5
Walaji: 1

Supu ya Kuku
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.