Biscuits za raspberry

Biscuite hizi ni tamu na rahisi kuandaa.

Mahitaji

 • Unga kikombe 1 na nusu 
 • Raspberry flavoured custard powder robo kikombe 
 • Baking powder kijiko 1 na robo
 • Sukari robo tatu ya kikombe
 • Raspberry kijiko 1 na nusu cha chai
 • Butter 150g
 • Maziwa vijiko 2 vya chakula
 • Iriki robo kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Biscuite hizi zimeandaliwa na Maria Rwegasira

 • Pasha oven nyuzi joto 180, Chukua bakuli, weka butter, ongeza sukari kisha changanya vizuri ilainike. Ongeza unga, custard powder, iriki na baking powder kwenye mchanganyiko wenye butter, changanya vizuri.
 • Weka maziwa na raspberry extract, kanda mpaka unga uchanganyikane vizuri.
 • Kata unga, sukuma kwenye meza au kibao cha chapati, chukua vifaa vya kukatia vya design tofauti kama picha inavyoonyesha kata shape unazotaka, oka kwa dakika 15, vitoe acha vipoe pembeni vikipigwa upepo vitakua crunchy.
 • Pia unaweza kuweka rangi au Nutella kupata radha tofauti, jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi za kuunga na nazi
dakika 20
Walaji: 2

Supu ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.