Broccoli ya bamia

Broccoli ni mboga rahisi kuandaa na yenye virutubisho muhimu vilivyo na faida kubwa mwilini. Mfano, broccoli inahusishwa zaidi na kuufanya mwili kuzuia kupatwa na saratani na vilevile kusafisha uchafu mwilini. Ni vizuri ukipendelea kula hiki chakula cha afya bora

Mahitaji

 • Broccoli
 • Karoti 2
 • Pilipili hoho 3
 • Vitunguu 2
 • Mafuta ya kula (binafsi nimetumia mafuta ya mizeituni, au olive oil)
 • Chumvi
 • Pilipili manga
 • Unaweza kuongeza viungo unavyopendelea (mfano: Hiliki, kitunguu saumu n.k)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Tunaandaa mboga ya broccoli iliyochanganywa na mboga tofauti za majani. Tukimaliza itakuwa inaonekana hivi.

20150201_190244

1. Andaa sauce ya mboga za majani

 • Andaa bamia, pilipili hoho, kitunguu na karoti kwa kuosha na kisha kukata vipande vidogo vidogo. Mie hupendelea vipande virefu na vyembamba.

20150201_172747

 • Bandika chungu jikoni, weka mafuta ya kula. Acha yapate moto vizuri.
 • Weka kitunguu, acha kilainike kiasi, kisha weka bamia. Koroga na acha vikaangike kwa muda wa dakika 3 hadi 4. Bamia huchelewa kuiva, hivyo ni vizuri ukiweka mwanzo wakati wa mapishi.

20150201_182828

 • Weka karoti, koroga vizuri. Weka pilipili hoho na endelea kukoroga. Funika na mfuniko kwa muda wa dakika 3 hadi 5. Mboga za majani hutoa maji, hivyo mboga itaiva na mvuke wake.
 • Unaweza kuongeza viungo unavyopenda hapa, mie naweka supu ya kuku au kiungo chochote cha nyama ili kuipa mboga ladha tamu na ya kipekee. Mie nimeweka pilipili manga na knorr sauce ya kuku, ili kupata ladha tamu.

20150201_183229

2. Andaa broccoli

 • Broccoli inaweza kupikwa kwa mapishi tofauti, hapa tunaangalia njia ya kupika kwa kutumia mvuke.

20150201_181617

 • Osha na kisha kata broccoli kwenye vishina vyake na ubaki na broccoli zenye vifungu vichache.
 • Weka broccoli kwenye chombo unachoweza kupikia kwa mvuke. Nyunyizia chumvi kiasi na weka kwenye jiko ili mvuke upate kuivisha.

Kama una rice cooker ni rahisi kutumia kile chombo chenye matundu, ni maalum kwa mapishi kama haya.

20150201_184244

 • Acha broccoli ipate mvuke kwa muda wa dakika 3 hadi 5. Kisha itoe.
 • Changanya brocolli na mboga nyingine za majani ulizoandaa na kisha acha ikae jikoni kwa dakika 3 hadi 4 ili zipate kuchanganyika vizuri.

20150201_190218

20150201_190237

20150201_190322

 • Baada ya muda mboga yako itakuwa tayari. Jirambe.

Faida za broccoli ni:

 • Kuondoa uchafu mwilini
 • Kukukinga na saratani

MAPISHI YAPENDWAYO

Cutlets za pilipili
dakika 5
Walaji: 4

Wali wenye nazi na maziwa
dakika 20
Walaji: 2

Nyama tamu yenye pilipili
dakika 25
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.