Brown rice, maziwa na karoti

Brown rice, chanzo cha wanga, protini na virutubisho vingine vingi. Ni chakula kizuri kwa familia nzima - watoto na watu wazima. Ni chakula kizuri sababu kina virutubisho asilia vinavyokupa afya bila kukupa madhara, tofauti na michele mingine.

Mahitaji

  • Mchele wa brown kikombe 1
  • Karoti 2
  • Maziwa vikombe 2
  • Chumvi kiasi
  • Sukari kijiko 1 cha chakula
  • Maji kikombe 1 na nusu
  • Mafuta kijiko 1 cha chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula hiki kimeandaliwa pamoja na maziwa. Maziwa ni kiungo kizuri kwenye wali, na humpa mtoto ladha tamu na kumfanya kufurahia chakula. Jaribu kumbadilishia mtoto chakula kwa kumuandalia vyakula vilivyo na ladha, lakini vinavyotumia viambato asilia.

Chakula hiki kimeandaliwa na @bubero.

  • Osha mchele, weka kwenye sufuria. Ongeza maji kisha bandika jikoni, moto wa wastani. Pika kwa dakika 20 au zaidi hadi mchele ulainike. Mchele wa brown huchukua muda mrefu kulainika tofauti na mchele mweupe. Maji yakikauka weka sukari, chumvi na maziwa kikombe 1. Acha chakula kichemke kwa dakika 15 zaidi.
  • Weka karoti - osha, menya kisha kwangua juu ya wali. Weka mafuta koroga kisha weka maziwa yaliyobaki na acha vichemke kwa dakika 10, ili karoti na mafuta viize.
  • Epua, pakua acha kipoe kidogo, tenga mpe mtoto ale.

misosi_brown_rice_main


MAPISHI YAPENDWAYO

Sambusa za limao na asali
dakika 30
Walaji: 5

Vipopo
dakika 30
Walaji: 4

Vitumbua vya iliki na nazi
dakika 35
Walaji: 8

Dagaa wenye curry sauce
dakika 25
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.