Butter chicken

Butter chicken unaweka pia kupika mchuzi, kuchoma au kukaanga na bado familia yako wakafurahia mlo huo.

Mahitaji

 • Kuku kilo 1 asiye na ngozi wala mifupa
 • Limao 1
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Pilipili manga ya kusaga vijiko 3 vya chakula
 • Tangawizi iliyosagwa kijiko 1 cha chai
 • Majani ya bay 3
 • Mdalasini uliosagwa kijiko 1 cha chai
 • Cardamon kijiko 1 cha chai
 • Butter vijiko 3 vya chakula
 • Vitunguu maji 2
 • Vitunguu saumu vijiko 5 vyakula
 • Giligiliani vijiko 2 vya chai
 • Cumin kijiko 1 cha chai
 • Garam masala kijiko 1 cha chai
 • Cayenne pepper kijiko 1 cha chai
 • Corn starch kijiko 1 cha chai
 • Olive oil kikombe 1 cha kahawa
 • Nyanya ya kopo vijiko 2 vya chakula
 • Maziwa mgando vijiko 2 vya chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa nyama ya kuku, isafishe vizuri iweke pembeni.
 • Chukua pilipili manga, tangawizi, majani ya bay, mdalasini, cardamon, maziwa mgando, vitunguu maji, vitunguu saumu, giligilian, cumin, garam masala, cayenne pepper na nyanya ya kopo.
 • Chukua blender weka hivyo vitu vyote kisha saga, hakikisha vimelainika kabisa na viungo vimechanganyikana vizuri.
 • Weka pembeni, chukua kuku mkate vipande vyenye umbo la mche mraba.
 • Chukua bakuli kubwa, weka kuku chukua ndimu kamulia, weka na chumvi. 
 • Mwagia mafuta ya olive oil kwenye kuku, changanya vizuri mpaka uone mafuta yameenea vizuri.
 • Chukua ule mchanganyiko ulioublendi mwagia kwenye kuku, weka na cornstarch, kisha changanya kwa usafaha mpaka uone kuku kaenea viungo.
 • Ukimaliza weka kwenye jokofu kwa lisaa 1, mtoe kuku mpake butter changanya kisha rudisha tena kwenye jokofu.
 • Muache akae usiku mzima au masaa 8.
 • Mtoe chukua butter paka kwenye chombo utakacho okea kisha panga kuku wako vizuri, au unaweza choma pia paka butter kwenye wavu wa kuchomea.
 • Choma huku unamgeuza na unampaka butter mpaka aive, na kwenye oven fanya hivyo hivyo. 
 • Dakika 45 zikifika mtoe atakua kaiva. Jirambe. Na uhakika huyu kuku atafurahiwa na familia yako.

MAPISHI YAPENDWAYO

Chicken tandoori
dakika 40
Walaji: 2

Chocolate cake
dakika 40
Walaji: 6

Sambusa za nyama
dakika 15
Walaji: 10

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.