Caramel cheese cake

Mahitaji

 • Cream cheese 340 g
 • Sukari nyeupe 330g
 • Butter nusu kikombe
 • Graham cracker cumbs vikombe 2(hizi ni kama buscuit)
 • Mayai 3
 • Vanila vijiko 2 vya chai
 • Caramel cubes kikombe 1
 • Caramel sauce nusu kikombe
 • Maziwa vijiko 5 vya chakula
 • Unga vijiko 2 vya chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Pasha oven nyuzi joto 175, paka mafuta chombo unachotumia kuokea.
 • Chukua graham cracker weka kwenye blenda na sukari vijiko 2, saga mpaka ilainike. Pima vikombe 2
 • Chukua bakuli weka graham cracker uliyosaga weka na butter koroga ichanganyike vizuri kisha weka kwenye chombo cha kuokea, weka na cubes za caramel oka kwa dakika 30.
 • Itoe iache ipoe,  chukua bakuli weka cream cheese, mayai, vanila, sukari na unga vijiko 2 changanya mpaka ilainike vizuri, kisha mwagia kwenye ule mchanganyiko ulio uoka mwanzo.
 • Chukua caramel weka maziwa bandika jikoni weka moto mdogo sana. Kisha mwagia juu ya ule mchanganyiko.
 • Oka kwa dakika 45 itoe, iache ipoe kwa dakika 15,kisha mwagia caramel iliyobaki kwa juu kisha kata wape watu wajirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya pilipili
dakika 15
Walaji: 2

Chips mayai na mboga za majani
dakika 20
Walaji: 2

Mishikaki ya kupaka
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.