Nguru wa kuchoma

Nguru ni aina ya samaki wa maji chumvi. Kama tunavyojua samaki wanatupatia madini ya chuma na protein. Unaweza kula na ugali, wali, mwenyewe au na chakula chochote na mkamfurahia.

Mahitaji

 • Nguru fillet
 • Vitunguu saumu
 • Parsley vijiko viwili vya chai
 • Olive oil vijiko 2 vya chakula
 • Ndimu kikombe kimoja cha kahawa
 • Chungwa kikombe kimoja cha kahawa
 • Pilipili manga/ pilipili ya kusaga vijiko 3 vya chai
 • Soy sauce kikombe kimoja cha kahawa
 • Oregano leaves nusu kijiko cha chai
 • Majani ya rosemary

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chukua bakuli, weka juice ya chungwa, soy sauce, olive oil, juice ya ndimu, pilipili manga, weka majani ya parsley, majani ya oregano, kitunguu saumu na rosemary kisha koroga mpaka vichanganyike vizuri.
 • Weka nguru, funika kile chombo chenye nguru na viungo weka kwenye fridge kwa nusu saa.
 • Washa jiko, paka wavu wa kuchomea mafuta. Kisha panga nguru juu.
 • Pika kwa muda wa dakika 4 unageuza upande wa pili, kila ukigeuza paka ile sauce iliyobaki kwenye bakuli.
 • Ukiona wameiva ni muda wa kujiramba na familia au marafiki.

MAPISHI YAPENDWAYO

Togwa
dakika 30
Walaji: 4

sweet and sour chicken
dakika 25
Walaji: 2

Caramel cheese cake
dakika 60
Walaji: 5

Mkate wa zucchini na korosho
dakika 55
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.