Chapati tamu za iliki na maziwa

Utamu wa chakula ni pale unapoweka mdomoni na kinakupa raha ya kukitafuna kwa muda mrefu zaidi ili kupata vionjo vyote muhimu vilivyomo. Uwepo wa iliki na maziwa kwenye chapati hizi hukupa ladha murua inayokufanya ufurahie zaidi chakula chako. Mapishi haya ni rahisi na matokeo yake hayana mfano.

Mahitaji

 • Unga wa ngano kilo 1
 • Mayai 2
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Maji
 • Siagi (butter) vijiko 3 vikubwa
 • Mafuta ya kula kwa ajili ya kuchomea
 • Iliki ya unga kijiko 1 kikubwa
 • Maziwa ya unga vijiko 3 vikubwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuandaa chapati hizi kisha ukahifadhi na kula wakati unaopenda. Hakikisha umehifadhi vizuri kwenye mifuko laini ya plastic ili iwe na unyevunyevu unaotakiwa.  

 • Kwenye beseni au sufuria kavu weka unga, chumvi, maziwa vijiko 3 vya chakula na iliki. Changanya pamoja hadi kila kitu kiwe kimechanganyika vizuri.
 • Weka siagi vijiko vitatu kwenye mchanganyiko wenye unga kisha changanya zaidi hadi siagi ishikane vizuri na unga.
 • Pasua mayai pembeni, yakoroge vizuri na kisha weka kwenye unga. Changanya zaidi hadi upate uwiano unaofaa.
 • Ukiona uwiano mzuri wa unga wako, weka maji ya uvuguvugu kwenye unga na anza kukanda. Kanda dida la chapati (mchanganyiko wa unga na maji) hadi uwe laini kabisa na haushikani na chombo unachokandia wala haunati kwenye mikono. Hapo unga utakua tayari kukupa chapati laini na tamu. Hii inachukua takribani dakika 20.

MUHIMU: Hakikisha unga umekandwa vizuri na umekuwa laini kabla ya kuuacha. Hii ndio hatua muhimu zaidi kuliko zote. Unaweza kuchukua takribani dakika 20 ili kumaliza hatua ya ukandaji, hivyo kuwa na subira ili kupata matokeo mazuri.

 • Kata mabonge ya unga kwa umbo la mviringo kisha weka kwenye chombo pembeni. Rudia hili zoezi hadi unga uishe.
 • Chukua donge mojamoja, paka unga weka kwenye kibao cha kusukumia chapati, sukuma chapati vizuri hadi iwe na umbo zuri duara bapa. Paka mafuta kwenye chapati na anza kukunja.
 • Rudia hilo zoezi kwa madonge yote yaliyobaki. Ukimaliza, anza kusukuma chapati zako kwa ajili ya kupika.
 • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri.
 • Weka chapati, acha iive hadi iwe rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili, paka mafuta kidogo sana upande uliokua wa kahawia kwa kutumia kijiko huku ukisambaza vizuri yaenee chapati nzima. Geuza, paka mafuta tena upande mwingine. Mafuta husaidia kuifanya chapati iwe laini na isipasuke kirahisi. Hii itasaidia kupata chapati tamu na laini, hasa wakati wa kula.
 • Hakikisha chapati inaiva vizuri na inachambuka.
 • Rudia zoezi hili hadi dida lako liishe. Hapo utakuwa umemaliza kazi na tayari kula chapati zako.
 • Unaweza kula chapati hizi na vyakula aina tofauti, mfano unaweza kula na mchuzi mtamu, chai, vinywaji baridi na vingine. Jirambe na chapati tamu.

misosi-chapati-iliki


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi za hiliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Ndizi za kuunga na nazi
dakika 20
Walaji: 2

Supu ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.