Chapati za maji zilizo na maziwa, vanilla na karoti

Chapati za maji ni tamu, hizi zinaongezewa utamu kwa kuwekewa viungo zaidi. Unapata virutubisho zaidi, si vya ngano tu, bali kuna protini inayotoka kwenye mayai na harufu nzuri inayotokana na vanila.

Mahitaji

 • Unga wa ngano kilo 1.
 • Sukari kijiko 1 cha chai.
 • Mayai 2.
 • Karoti 2.
 • Kitunguu maji
 • Chumvi ½ kijiko cha chai.
 • Vanila
 • Cream ya maziwa
 • Maji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Weka unga wako kwenye chombo kikavu. Ongeza sukari na chumvi weka kidogo sana.
 • Kwangua carrot zako ila zitoke zipande vidogo vidogo sana. Kata vitunguu vipande vyembamba. Tenganisha vitunguu ili visije kushikana.
 • Weka vitunguu na karoti kwenye unga. Koroga mchanganyiko na mikono (Hakikisha mikono yako ni misafi)
 • Mchangayiko ukishakuwa sawia, ongeza maji kiasi kisha endelea kukoroga unga. Angalia uwiano wake, usiwe mzito sana wala mwepesi sana. Ongeza maji ili kupata mchanganyiko sawia.
 • Pasua mayai na weka kwenye mchanganyiko kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe sawia.
 • Weka cream ya maziwa kisha koroga vizuri.
 • Weka ½ kijiko cha vanila kisha koroga. Vanila inahitajika kuongeza harufu, usiweke nyingi sana.
 • Bandika kikaangio chako jikoni (frying pan). Ikipata moto, chota mchanganyiko na weka kwenye kikaangio. Unaweza kutumia kikombe au upawa kufanya zoezi hili.
 • Weka rojo ya unga wako kwenye kikaangio chako (fryin pan) uwe na umbo la duara kama chapati.
 • Ikikauka geuza na weka mafuta, kisha geuza upande wa pili angalia kama imeiva unatoa hapo tayari kwa kuliwa.

MAPISHI YAPENDWAYO

Vipopo
dakika 30
Walaji: 4

Vitumbua vya iliki na nazi
dakika 35
Walaji: 8

Dagaa wenye curry sauce
dakika 25
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.