Cheese Burger

Kuna wale wanaopenda kula burger, lakini cha muhimu ni kula chakula kinachoboresha afya yako zaidi na siyo kuharibu. Ni vizuri kama utakula burger unayoandaa mwenyewe kwa kutumia viungo bora unavyopendelea. Ni chakula chepesi, unaweza kuandaa kwa kutumia mboga za majani kwa afya zaidi, au kwa aina ya nyama unayopenda.

Mahitaji

 • Nyama ya kusaga gramu 400
 • Kitunguu 1, kata vipande vidogo
 • Mikate 4 (Au scones) unayotumia kwa burger
 • Chumvi, pilipili, viungo kwa ajili ya ladha
 • Cheese vipande 4, viwe vyembamba vipana
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Olive oil

Mahitaji ya sauce

 • Haradali (Mustard) 1/2 kijiko kidogo
 • Mayonnaise vijiko 4 vikubwa

Salad

 • Tango 1, kata vipande vyembamba
 • Nyanya 2, kata vipande vyembamba vya uviringo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza mahitaji kutokana na unavyopenda.

misosi-cheese-burger-main1

Andaa sauce

 • Changanya mayonnaise na haradali kwenye bakuli. Koroga vizuri hadi ichanganyike vizuri.

Andaa burger

 • Kaanga nyama ya kusaga kwenye kikaango. Weka viungo ili kuipa ladha – pilipili manga, chumvi, kitunguu, na viungo vingine unavyopendelea kwenye nyama.
 • Tengeneza nyama kwenye umbo la uviringo, nyama iwe na umbo na ukubwa sawa na mikate unayotumia kwa burger. Pika hadi iive vizuri.
 • Kata mikate katikati, pasha moto vizuri. Unaweza kutumia microwave kupasha moto.
 • Kwenye kipande kimoja cha mkate, panga cheese, nyama, vipande vya nyanya na tango, mwagia sauce kisha funika na upande mwingine wa pili.
 • Malizia burger zilizobaki, kisha jirambe.
 • Unaweza kula burger na chips au salad, inategemea chaguo lako.

misosi-cheese-burger-insta-0


MAPISHI YAPENDWAYO

Creamy rice pudding
dakika 60
Walaji: 2

Nyama ya mbuzi ya kukaanga
dakika 20
Walaji: 2

Nyanya chungu na bamia
dakika 10
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.