Chicken bread filling ( Nyama ya kujazia mkate wa kuku)

Nyama hii imtengenezwa maalum kwa ajili ya kujazia kwenye mkate wa kuku.

Mahitaji

 • Minofu ya kuku ¼ kilo
 • Kitunguu 1 kilichokatwa vipande vidogo
 • Majani ya Korianda
 • Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili ndogo za kijani, zikate vipande vidogo
 • Masala Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili manga
 • Unga vijiko 2 vikubwa
 • Kikombe 1 cha maziwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Nyama hii imtengenezwa maalum kwa ajili ya kujazia kwenye mkate wa kuku. 

 • Kata vipande vya nyama ya kuku (minofu), chemsha hadi iive vizuri na supu ikauke.
 • Toa nyama, hifadhi pembeni. Ikishapoa, iponde ponde ili iwe vipande vidogo vidogo

20150117_135416

 • Bandika kikaango, weka mafuta. Acha yapate moto.
 • Weka kitunguu. Koroga hadi kigeuke rangi na kiwe laini.
 • Weka unga, chumvi, pilipili manga, na masala. Koroga pamoja kama dakika 2 hadi 3.

20150117_140329

 • Weka maziwa, koroga vizuri. Acha iive kiasi hadi iwe uji mzito.
 • Weka pilipili za kijani, ongeza majani ya korianda. Koroga vizuri.

20150117_140509

20150117_140626

 • Weka kuku. Koroga vizuri.
 • Bandua toka jikoni. Hifadhi pembeni acha ipoe.
 • Mchanganyiko wako utaonekana kama hivi.

20150117_141145


MAPISHI YAPENDWAYO

Nyama ya kuoka na ndizi mzuzu
dakika 45
Walaji: 2

Kuku wa kuoka na tambi
dakika 45
Walaji: 2

Mboga ya majani mchanganyiko
dakika 10
Walaji: 4

Omelette za pilipili hoho
dakika 5
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.