Chicken Curry

Curry sauce ni mboga nzuri kwa kula na vyakula tofauti. Ladha yake inakupa hamu tosha ya chakula. Hii curry sauce ilipikwa bila kutumia nyanya. Mchuzi ulikuwa mzito sababu nilitumia tui zito la nazi vikombe 2. Kuku alikuwa mtamu, ananukia vizuri na anapendeza kumuangalia.

Mahitaji

 • Kuku ½
 • Kitunguu maji kikubwa 1
 • Punje 6 za kitunguu saumu, kata vipande vidogo
 • Tangawizi 1, menya kisha saga
 • Mafuta ya kula
 • Mdalasini, mti 1
 • Pilipili nyekundu kijiko 1 kidogo
 • Pilipili hoho 1
 • Curry powder
 • Korianda kijiko 1 kidogo
 • Tui la nazi vikombe 2
 • Chumvi
 • Limao au ndimu 1
 • Cayenne pepper

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kula curry sauce na vyakula mbali mbali, mfano ugali, wali, chapati, ndizi, maandazi au chochote unachopenda.

 misosi_recipe_curry_main

 • Andaaa kuku – kata vipande  vinavyotosha kisha osha na hifadhi kwenye chombo safi.  Weka chumvi, nyunyizia limao. koroga vizuri ili vienee kwenye nyama. Weka tangawizi, koroa vizuri pamoja. Acha pembeni  ipate kuingia vizuri viungo.
 • Andaa kitunguu maji na kitunguu saumu – menya kisha kata vipande vidogo. Osha kisha kata pilipili hoho na cayenne pepper vipande vidogo. Hifadhi pembeni.
 • Bandika kuku jikoni, usiweke maji kwenye kikaango. Acha kuku achemke hadi maji yakauke. Ongeza maji kikombe 1 na nusu ili kuku aive vizuri.
 • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto, kisha weka mafuta ya kula. Yakipata moto, weka kitunguu saumu, kitunguu maji. Koroga vizuri hadi viive. Weka pilipili hoho na cayenne pepper kisha koroga vizuri. Acha viive. Kama kukiwa hakuna mchuzi, weka supu ya kuku kiasi kwenye mboga za majani. Koroga kisha funika kidogo viive vizuri -takribani dakika 3.
 • Changanya kuku na mboga za majani kwenye chombo kimoja. Koroga vizuri. Weka curry powder vijiko 2 vikubwa, koroga. Weka kila kiungo kilichobaki, kasoro tui la nazi. Koroga vizuri kwa pamoja.
 • Mimina tui la nazi kwenye sufuria yenye kuku. Koroga hadi tui lichemke, usiache kukoroga maana tui litakatika. Acha mboga ichemke hadi iive vizuri.
 • Epua na tenga chakula ili upate kujiramba kwa nafasi yako.

misosi_chicken_curry_main


MAPISHI YAPENDWAYO

Mtori wa ndizi
dakika 45
Walaji: 1

Pilipili ya maembe ya kusaga
dakika 35
Walaji: 5

Chicken with mashed potato
dakika 30
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.