Chicken Tandoori

Ulishawahi kula chicken tandoori? Huyu kuku unaweza kumla hadi mifupa, maana utamu wake unakuwa umezidi. Ni rahisi kuandaa na unaweza kula wakati wowote.

Mahitaji

 • Kuku vipande 4
 • Tandoori sauce
 • Tangawizi ya unga kitunguu
 • Kitunguu saumu 1
 • Chumvi
 • Limao au ndimu 1 au unaweza kutumia vinegar
 • Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive oil)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chicken tandoori, unaweza kuongea au kupunguza viungo ili kupata ladha unayotaka. 

 • Andaa kuku, kata vipande vinavyotosha kisha osha vizuri. Usitoe ngozi ili isaidie nyama kuiva vizuri wakati wa kuoka. Nyunyizia chumvi kwenye kuku. Hifadhi pembeni.
 • Andaa marinade. Kwenye bakuli – kamua limao au ndimu,  weka kitunguu saumu, tangawizi na tandoori sauce. Koroga vizuri hadi vichanganyike vizuri. Chovya vipande vya kuku kimoja baada ya kingine kwenye marinade. Hakikisha umepaka sauce vizuri kwenye nyama, kati ya nyama na ngozi. Rudia vipande vyote hadi umalize. Unaweza pia kuloweka vipande kwenye sauce kama iko nyingi. Hifadhi nyama kwenye jokofu kwa muda wa saa 1 hadi 2 ili viungo vipate kuingia vizuri.
 • Washa oven, weka nyuzijoto 200°C (392°F) kwa muda wa dakika 10.
 • Paka mafuta kiasi juu ya nyama na kati ya ngozi na nyama. Mafuta yanasaidia kuifanya nyama iive bila kukauka na kuwa ngumu.
 • Panga nyama vizuri kwenye wavu wa kuokea, hakikisha kuna nafasi vizuri kati ya nyama. Weka nyama kwenye oven, tega muda wa dakika 50 hadi 60 ili nyama ipate kuiva. Kama oven inatoa joto chache kwa chini, geuza nyama kila baada ya dakika 15 ili iive vizuri  pande zote.
 • Baada ya dakika 50 hadi 60 angalia kama nyama imeiva vizuri na imechuja maji yote. Epua na tenga ujirambe.

misosi-chicken-tandoori-mai


MAPISHI YAPENDWAYO

Mtori wa ndizi
dakika 45
Walaji: 1

Pilipili ya maembe ya kusaga
dakika 35
Walaji: 5

Chicken with mashed potato
dakika 30
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.