Chicken tandoori

Chicken tandoori ni chakula kitamu sana, asili yake ni india. Kuku huyu waweza kumla mwenyewe au ukala na chakula chochote na ukafurahi

Mahitaji

 • Kuku vipande 6 visivyo na ngozi
 • Maziwa mgando nusu kikombe
 • Limao 2
 • Paprika nusu kijiko cha chai
 • Kitunguu saumu kilichosagwa vijiko viwili vya chakula
 • Tangawizi iliyosagwa vijiko viwili vya chakula
 • Jira kijiko kimoja cha chakula
 • Coriander kijiko kimoja cha chai
 • Cayene pepper nusu kijiko cha chai
 • Cardamon robo kijiko cha chai
 • Karafuu iliyosagwa robo kijiko cha chai
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chakula
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Mafuta ( olive oil) vijiko saba vya chakula
 • Majani ya fenugreen kijiko 1 cha chakula
 • Garam masala nusu kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chukua bakuli,weka maziwa mgando, limao, vitunguu saumu, tangawizi, jira, coriander, cayenne pepper, cardamon, karafuu, pilipili manga na chumvi.
 • Changanya vizuri, vichanganyike kwa ufasaha.
 • Ukiona imechanganyika, ongeza garam masala, fenugreen na paprika endelea kuchanganya.
 • Weka kuku ndani ya ule mchanganyiko, hakikisha ameenea viungo. Ni vizuri ukimchana chana kuku kuruhusu viungo kuingia.
 • Endelea kumgeuza kuku kwenye viungo mpaka uhakikishe kaenea kwenye viungo.
 • Chukua mfuko wa nailoni ulio laini, weka kuku na ule mchanganyiko.
 • Funga weka kwenye jokofu, muache kwa masaa 9 au alale kwenye jokofu usiku mzima.
 • Mtoe kuku nusu saa kabla ya kupika,mpake mafuta. Paka mafuta na kwenye chombo unachoenda kumpikia kuku.
 • Panga kuku vizuri kwenye pan ya kuomea.
 • Pik kwenye oven kwa dakika 35. Akiiza mtoe muanze kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Cornbread yenye korosho
dakika 40
Walaji: 6

Bata wa mchuzi wenye Bizari
dakika 40
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.