Chicken wings (Vipapatio vya kuku)

Ukipenda kula kuku wa kukaanga, basi huyu ndio anafaa. Chicken wings hizi unaweza kuzipika na kula kama kitafunwa wakati wa kupumzika na familia au wakati wa vikao muhimu na marafiki.

Mahitaji

Mahitaji ya msingi

 • Vipapatio vya kuku 10 (Unaweza kuwa na idadi yeyote, kutegemea na walaji)
 • Vijiko 5 vya sauce ya pilipili (Unaweza pia kuwa na pilipili ya kuongezea)
 • Siki iliyochujwa (distilled Vinegar)
 • Mafuta ya kukaangia (Vizuri kama ukiwa na mafuta yanayotokana na mimea)
 • Vijiko 4 vya majarini (siagi au margarine)
 • Chumvi
 • Pilipili (hii ya kuongeza utamu)
 • Pilipili manga

Vitu vya ziada kwa kuku (si lazima)

 • Kitunguu saumu cha unga
 • Tangawizi
 • Limao

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya ni maalumu kwa chicken wings, ila mie nilipika kuku mzima kwa style hii, hivyo usishangae ukikuta vipaja na vitu vingine. Kwa upishi huu unaweza kupika kuku mzima, ila ni maalum kwa vipapatio (wings).

Tunatengeneza hiki chakula katika sehemu mbili tofauti - tutakaanga kuku, wakati huo huo tutapika sauce yetu ya pilipili. Tukimaliza, mapishi yatakuwa yanaonekana kama hivi:

20150124_213633

 • Hii hatua si lazima, ila mie binafsi huwa napenda kuwawekea viungo kuku nnaowapika, hasa wale ambao siwachemshi kabla ya kuwakaanga, maana kuku anachukua muda kuiva, hivyo ni vizuri kuweka viungo ili alainike na kuiva vizuri wakati wa kumkaanga. Kwa hiyo, ningeweka kitunguu saumu, limao na tangawiki kisha niwaache kwa dakika 15 hadi 20 kabla ya kuwakaanga. Ila hii hatua si lazima, hivyo unaweza kuanza kukaanga kuku bila kuwawekea viungo zaidi ya chumvi tu, na watatoka vizuri kabisa.

20150124_202103

20150124_203013

 • Weka mafuta jikoni kwenye chombo kinachotosha. Acha yapate moto vizuri, kisha weka vipande vya kuku.

20150124_204053

 • Acha kuku waive vizuri hadi wakauke na kubadilika rangi. Inachukua kama dakika 10 hivi. Toa kuku na weka kwenye tissue paper, ili wachuje mafuta vizuri. Rudia hatua hii kwa vipande vilivyobaki.

20150124_205750

 • Weka chombi jikoni, weka majarini na uache iyeyuke vizuri.

20150124_204126

 • Ongeza siki (vinegar) na kisha koroga vizuri.
 • Weka sauce ya pilipili. Koroga vizuri. Usiache kukoroga maana inaweza kuganda na kuunga.
 • Unaweza kuongeza chumvi na pilipili kwenye sauce ili kuongeza ladha.

20150124_204802

 • Fahamu kuwa, muda mrefu hii sauce inavyokaa jikoni ndio inavyozidi kuwa kali. Hivyo basi, kama hupendi ukali sana, toa jikoni baada ya muda kiasi. Na kama unahitaji pilipili zaidi ongeza vipimo.
 • Ukimaliza tenga na jirambe na kuku wako.

20150124_213546

20150124_213644

20150124_213724


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.