Chicken Wings zilizopakwa Mayai

Hizi chicken wings zinachovya kwenye mayai kisha kukaangwa kwa muda mfupi kwenye siagi. Baada ya kukaanga vinachovywa kwenye sauce na kisha kuokwa. Zikiiva utapata ladha tamu ya chicken wings laini na tamu.

Mahitaji

 • Vipapatio vya kuku kilo 1
 • Yai 1, pasua na vuruga
 • Kikombe 1 cha unga wa ngano, kwa kuweka utando (layer) juu ya kuku
 • Kikombe 1 cha siagi (butter)

Mahitaji ya sauce

 • Vijiko 3 vikubwa vya soy sauce
 • Vijiko 3 vikubwa vya maji safi na salama
 • Kikombe 1 cha sukari
 • ½ kikombe cha white vinegar
 • ½ kijiko kidogo cha kitunguu saumu cha unga
 • Kijiko 1 kidogo cha chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hizi chicken wings zinachovya kwenye mayai kisha kukaangwa kwa muda mfupi kwenye siagi. Baada ya kukaanga vinachovywa kwenye sauce na kisha kuokwa. Zikiiva utapata ladha tamu ya chicken wings laini na tamu.

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 350 degrees F (175 degrees C), acha ipate moto.
 • Kata vipapatio vya kuku (chicken wings) katikati, chovya kwenye mayai na kisha chovya kwenye unga. Hakikisha mayai na unga vimeenea vizuri.
 • Bandika chombo jikoni kwenye moto wa wastani, acha kipate moto kisha weka butter. Acha iyeyuke. Weka vipapatio ya kuku na kanga hadi vibadilike rangi. Epua na weka kwenye waya wa kuokea.
 • Kwenye bakuli ya wastani, changanya soy sauce, maji, sukari, vinegar, kitunguu saumu, na chumvi. Koroga vizuri hadi mchanganyiko uwe sawia. Nyunyizia sauce juu ya vipapatio vya kuku.
 • Weka vipapatio kwenye oven, oka kwa muda wa dakika 30 to 45. Weka sauce juu ya vipapatio mara kwa mara. Vikiiva epua na weka pembeni.
 • Jirambe na ladha tamu ya japanese chicken wings.

chicken-wings-misosi-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Viazi lishe, karoti na maziwa
dakika 20
Walaji: 1

Wali wa viungo
dakika 20
Walaji: 4

Tambi za sausage na kuku
dakika 45
Walaji: 2

Kuku wa kuoka na ndizi mzuzu
dakika 60
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.