Chicken wrap

Chicken wraps ni chakula rahisi na chepesi kula. Mara nyingi hiki chakula kinaliwa kikiwa cha baridi. Hivyo ni chakula muafaka cha kuandaa ili kwenda kula ofisini au shuleni. Unaweza pia kuhifahi kwenye jokofu kwa muda mrefu baada ya kuandaa na kula wakati unaopenda.

Mahitaji

 • Tortilla 4
 • Minofu ya kuku Gramu 400 g
 • Salad gramu 400 g,  mie nimetumia kabichi, unaweza kuchagua majani unayopendelea
 • Nyanya 1
 • Mayonnaise au haradali (mustard) vijiko 2 vikubwa
 • Viungo – kitunguu saumu, chumvi, pilipili manga

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 

Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kama upendavyo.

misosi-wraps-2

 • Andaa nyama ya kuku. Kata vipande vidogo, osha kisha weka kwenye sufuria. Weka chumvi, kitunguu saumu na tangawizi, koroga vizuri viungo viendee kwenye nyama. Bandika jikoni,usiweke maji. Acha nyama ichemke hadi maji yakauke. Ongeza maji kama ½ lita ili nyama iive vizuri hadi ilainike. Maji yakikauka, epua nyama, hifadhi pembeni. Acha ipoe vizuri kisha kata vipande vidogo vidogo vinavyofaa kuliwa. Hifadhi pembeni.
 • Anza kupaka mayonnaise (au haradali) juu ya tortilla. Hakikisha imeenea vizuri.
 • Kata nyanya vipande vyembamba na vidogo. Toa mbegu za ndani. Nyunyizia chumvi kwa juu. (Unaweza kuongeza tango na karoti kama unapendelea)
 • Kata majani na tandaza juu yake. Nyunyiza pilipili ya unga juu yake kisha funga vizuri kwa kuzungusha kwenye umbo la uviringo, lisifunguke kirahisi. Hifadhi kwenye mfuko wa plastiki na weka kwenye jokofu (fridge).
 • Rudia hatua hii kwa wraps zilizobaki. Kata umbo la mshazari (diagonal), au unaweza kula kama ilivyo.
 • Jirambe na chicken wraps.

misosi-wraps-0


MAPISHI YAPENDWAYO

Mishikaki mitamu yenye papai
dakika 30
Walaji: 6

Kababs za kuku na mayai
dakika 20
Walaji: 4

Macaroni ya bilinganya na nazi
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.