chilli chicken

Mahitaji

 • Kuku
 • Corn flour vijiko 2 vya chakula
 • Pilipili manga nusu kijiko cha chai
 • Chumvi
 • Soy sauce vijiko 2 vya chakula
 • Mafuta
 • Vitunguu saumu
 • Tangawizi
 • Pilipili mbuzi 2
 • Vitunguu maji 1
 • Vinegar kijiko 1 cha chai
 • Sukari kijiko 1 cha chai
 • Supu ya kuku au maji nusu kikombe
 • Chilli sauce vijiko 2 vya chakula
 • Majani ya vitunguu maji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Msafishe kuku vizuri, muweke kwenye bakuli.
 • Weka pilipili manga, corn flour, chumvi, soy sauce na mafuta. Changanya vizuri sana.
 • Bandika mafuta jikoni, yakipata moto weka kuku, kuku akianza kubadirika rangi geuza uwatoe.
 • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta yakipata moto, weka tangawizi na kitunguu saumu, koroga. Weka pilipili mbuzi hizi zikate kate koroga, zikianza kubadilika rangi weka vitunguu maji.
 • Huku ukiendelea kukoroga weka soy sauce na chilli sauce  kisha weka kuku endelea kukoroga.
 • Weka chumvi,sukari endelea kukoroga, weka maji acha yachemke kabisa kisha weka vitunguu vya kijani na vinegar.
 • Acha ichemke kama dakika tano weka corn flour ila changanya na maji kwanza, acha ichemke kama dakika 7.
 • Ukiona maji yamekauka kabisa, weka chilli sauce na changanya vizuri. epua jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Karanga za mayai
dakika 10
Walaji: 10

Tambi na nyama ya kusaga
dakika 25
Walaji: 2

Chachandu ya embe
dakika 15
Walaji: 4

Bagia za kunde
dakika 7
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.