Chilly beef

Mahitaji

 • Nyama nusu kilo
 • Soy sauce vijiko 3 vya chakula
 • Chilly sause kijiko 1 cha chakula
 • Nyanya ya kopo 1 kijiko kimoja
 • Pilipili manga vijiko 2 vya chakula
 • Tangawizi
 • Vitunguu saumu
 • Pilipili mbuzi 3
 • Vitunguu maji 2 
 • Chumvi
 • Royco
 • Mafuta
 • Majani ya thyme na parsely
 • Unga wa mahindi nusu kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Pika nyama na chumvi mpaka iive, iweke pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni weka mafuta, tangawizi, kitunguu saumu, vitunguu maji na pilipili mbuzi zikate kate weka zote koroga kwa dakika5.
 • Weka nyama koroga, weka majani ya thyme koroga, weka soy sauce chill sauce na nyanya ya kopo, koroga kwa muda wa dakika7.
 • Weka unga koroga kwa dakika 2, pilipili manga, weka royco kisha weka majani ya parsely koroga ifunike dakika 3 kisha endelea kukoroga hapo itakua tayari sasa waweza kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Nyama ya kuoka na ndizi mzuzu
dakika 45
Walaji: 2

Kuku wa kuoka na tambi
dakika 45
Walaji: 2

Mboga ya majani mchanganyiko
dakika 10
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.