Chips dume za mayai na kuku

Chips dume ni upishi tofauti wa viazi unaoweza kuandaliwa kwa viungo mbalimbali na pia kuweka vionjo utakavyo. Mie napenda kuweka ladha mbalimbali, na kama katika hili pishi niliweka mchuzi wa kuku na mayai. Matokeo yake yalikuwa ni zaidi ya mazuri, na chakula nikala kwa kufurahia.

Mahitaji

 • ½ kilo ya viazi mbatata (Viazi mviringo au viazi ulaya)
 • Supu ya kuku (kidogo tu ili kuleta ladha, mie nilitumia kiporo nilichokuwa nacho)
 • Mafuta ya kula ¼ lita
 • Mayai 2
 • Chumvi
 • Pilipili manga ya unga
 • Kitunguu saumu cha unga

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ukitaka kujiramba kwa style hii, basi andaa chakula kinachofanana na hiki, halafu weka vikorombwezo unavyopenda mwenyewe. Mie nilikula pamoja na broccoli iliyoandaliwa kama ilivyoainishwa hapa.

20150202_175850

 • Menya viazi, osha na kisha kata katikati kisha hifadhi kwenye chombo chenye maji.
 • Weka chumvi kiasi kwenye viazi, bandika jikoni. Vikianza kuchemka, acha vikae kwa dakika 5 hadi 7, kisha ipua na weka pembeni. Kumbuka, havitakiwi kuiva sana, vinatakiwa kupata maji kiasi ili kuvilainisha, ila siyo kuiva kabisa.
 • Andaa supu kwenye chombo tofauti, tumbukiza viazi na koroga koroga ili vipate kuenea. Weka jikoni kwa muda wa dakika 3 hadi 5 ili vipate kuchemka kidogo na supu kuingia kwenye viazi.

20150201_173431

 • Pasua yai kwenye chombo kikubwa, kama bakuli, koroga vizuri. Weka pilipili manga ya unga, chumvi na kitunguu saumu. Koroga ili vipate kuchanganyika vizuri.
 • Mwagia viazi kwenye bakuli yenye mayai, koroga vizuri ili yapate kuchanganyikana vizuri.

20150201_174125

 • Bandika kikaangio, weka mafuta na acha yapate moto vizuri. Hakikisha mafuta ya moto vizuri kabla ya kuweka viazi, maana viazi vinaweza kuanza kubondeka kama vikikaa kwenye mafuta muda mrefu bila kuiva.

20150201_174305

 • Ukimaliza, tenga viazi kwenye tissue (paper towel) ili uchuje mafuta. Rudia kukaanga viazi vilivobaki hadi viishe.
 • Andaa chakua chako na ujirambe.
 • Unaweza kula viazi hivi kama vilivyo, kwa nyama choma, mishikaki, au na mboga mboga kama nilivyokula mie.
 • Usisahau kumshirikisha mwenzio kwenye maakuli haya matamu.

20150202_175757

20150202_175925

20150202_175907


MAPISHI YAPENDWAYO

Keki ya nanasi
dakika 40
Walaji: 4

Banana muffins
dakika 20
Walaji: 10

Uji wa mchele na ndizi
dakika 35
Walaji: 1

Creamy garlic potato
dakika 40
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.