Chips mayai na mboga za majani

Chips mayai ni chakula kinachopendwa sana kwenye jamii yetu. Kama hupendi chips mayai basi bado hujala hizi. Jaribu kujiramba na mapishi tofauti ya chips mayai zenye mchanganyiko wa mboga tofauti za majani. Kuwa makini usijing’ate, maana ni tamu hakuna mfano.

Mahitaji

 • Viazi ulaya 5 vikubwa
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu kikubwa 1
 • Mafuta ya kula
 • Chumvi
 • Mayai 4
 • Karoti
 • Kitunguu saumu
 • Nyanya

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya viazi, osha, kata vipande vidogo na uhifadhi kwenye maji. Ongeza chumvi ili kuvipa ladha mapema.
 • Bandika kikaangio jikoni, weka mafuta ya kula. Subiria yachemke vizuri.
 • Weka viazi na uanze kukaanga chips. Kuwa makini ziive vizuri zisije kuungua.
 • Wakati unakaanga chips anza kuandaa pilipili hoho, kitunguu na karoti. Osha, kata na kisha weka kwenye chombo tofauti pembeni. Menya kitunguu saumu na kukiponda vizuri.
 • Ukishamaliza kukaanga chips weka kwenye chombo tofauti pembeni.
 • Injika kikaangio tofauti cha kukaangia chips majai na ongeza mafuta kwenye kikaangio. Ni vizuri kama utatua kikaangio (frying pan) chenye muundo wa sahani ili kupata matokeo mazuri. Subiria mafuta yapate moto vizuri.
 • Weka nusu ya kitunguu kwenye kikaangio. Acha kiive. Kisha weka pilipili hoho na karoti. Koroga kiasi na acha kwa dakika 2. Kisha ongeza chips zilizoiva. Hakikisha bado kuna mafuta kiasi ya kutosha kukaangia mayai. Koroga mchanganyiko vizuri.
 • Pasua yai, koroga vizuri kisha ongeza kitunguu saumu kiasi. Bakisha kiasi kwa sababu ya mkupuo wa pili wa chips. Koroga na kisha ongeza kwenye kikaangio kwa utaratibu kufuatia umbo la kikaangio ili kueneza vizuri. Usikoroge, acha kwanza yai liive.
 • Yali likiiva upande mmoja unaweza kugeuza chips zako kwa kuzimimina taratibu kwenye sahani na kisha kuzigeuza kwa kuzirudishia kwenye kikaango upande mbichi ukiwa chini.
 • Subiria dakika chache na kisha epua chips zako na hifadhi kwenye chombo tofauti pembeni.
 • Rudia zoezi kwa sahani ya pili.
 • Ukimaliza unaweza kukata kachumbari ya kukipa ladha chakula chako.

Jirambe na utamu wa zege lenye kila aina ya utamu.


MAPISHI YAPENDWAYO

Kachori tamu zenye giligilani
dakika 20
Walaji: 6

Keki tamu ya mtindi na vanilla
dakika 50
Walaji: 8

Toa maoni yakofatma athuman
04:56, Sat 11 Oct 2014
Ni poa Nitaipika hii leo
Charlotte Misosi
07:04, Mon 13 Oct 2014
Karibu sana Fatma Athuman, ukishapika pishi hili naomba nipe matokeo yake. Najua utakuwa umefurahia, maana chips mayai ni chakula kizuri, hasa zile zinazoandaliwa tofauti na mapishi ya kila siku tuliyozoea. Mlo mwema :-)
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.