Chips na kuku

Chips zilizochanganywa na kuku, chakula hiki ni kizuri na rahisi kuandaa. Radha ya chakula hiki ni nzuri sana na utafurahia.

Mahitaji

 •  Kuku ½ kg
 • Viazi ulaya ½ kilo
 • Nyanya 2 kubwa zilizoiva vizuri
 • Kitunguu saumu ¼ kijiko cha chai
 • Tangawizi ¼ kijiko cha chai
 • Korianda ¼ kijiko cha chai
 • Hing ¼ kijiko cha chai
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai
 • Mafuta ya kula
 • Apple cider vinegar ½ kikombe cha kahawa
 • Oyster sauce vijiko 2 vya chakula
 • Kitunguu maji 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya viazi kisha kata ukubwa wa chips unaopenda. Hifadhi vizuri kwenye maji yaliyowekwa chumvi.
 • Safisha kuku vizuri kisha weka kwenye sufuria safi. Mwagia vinegar juu ya kuku. Bandika sufuria ya kuku jikoni. Acha ichemke vizuri. Kisha toa na hifadhi pembeni.
 • Bandika kikaango, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka viazi na kaanga hadi chips ziive. Epua na hifadhi pembeni. Rudia hadi viazi vyote viwe vimepikwa.
 • Kaanga kuku kwenye mafuta uliyotumia kupikia chips.
 • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta. Yakipata moto weka kitungu maji na viungo vyote ila usiweke nyanya na oyster sauce. Vitunguu vikianza kubadilika rangi weka nyanya. Nyanya zikiwa tayari weka kuku na funika vizuri kwa dakika 5 kisha weka oyster sauce. Ongeza supu ya kuku nusu kikombe kwenye sufuria, acha ichemke.
 • Weka chips kwenye sufuria lenye sauce ya kuku, pika hadi supu ikaukie.
 • Epua, tenga chakula na jirambe.

misosi-chips-kuku


MAPISHI YAPENDWAYO

Mille feuille pastry
dakika 25
Walaji: 6

Sambusa za limao na asali
dakika 30
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.