Chips na nyama ya ng'ombe

Chips hizi na nyama zinaandaliwa kwa viungo ili kuvipa ladha tamu. Chips zikipikwa hadi kukauka vizuri huwa na ladha ya kipekee na harufu ya kuvutia. Nyama hii ina ladha tamu, ubora wa kipekee na ikiiva vizuri inaweza kukufanya ujing’ate vidole wakati wa kula.

Mahitaji

 • Viazi ½ kilo
 • Chumvi
 • Tangawizi, ponda kwenye kinu, iwe laini.
 • Kitunguu saumu, ponda kwenye kinu, ilainike vizuri.
 • Pilipili manga ya unga
 • Nyama ¼ kilo
 • Magic cube 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza viungo kutokana na unavyopendelea. Hakikisha unatumia vizuri viungo maana vinatumika kwenye kuvipa ladha nyama na chips kwa pamoja. Hivyo usiweke vyote kwenye nyama na kutoweka kwenye viazi.

Andaa viazi

 • Menya viazi kisha weka kwenye chombo chenye maji mengi. Weka chumvi kiasi kwenye maji. Weka tangawizi iliyosagwa, kitunguu saumu kilichopondwa ili kuweka ladha na harufu tamu kwenye viazi. Hakikisha viazi vinakaa muda wote kwenye maji kabla ya kuvipika. Takribani dakika 20 zinatosha kuvipa ladha na harufu tamu.
 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta mengi. Acha yapate moto vizuri sana. Weka viazi kwa awamu acha hadi viive. Geuza ikiwezekana ili vipate kuiva vizuri. Hakikisha hurundiki viazi ili visigandiane.
 • Viazi vikiiva hifadhi pembeni kwenye paper towel (au kitambaa) ili kuchuja mafuta. Usifunike maana viazi vikifunikwa huharibika.

Andaa nyama

 • Tayarisha nyama – kata vipande vipana na vyembamba kisha osha vizuri. Weka chumvi, limao, ndimu au vinegar kwenye nyama. Changanya ili limao na chumvi viingie vizuri pande zote mbili.
 • Weka viungo vilivyobaki – chumvi, magic cube, tangawizi na kitunguu saumu kwenye nyama. Changanya nyama ili viungo vipate kuchanganyika vizuri. Acha nyama ikae kwa dakika 40 kwenye jokofu ili viungo viingie vizuri. Jinsi viungo vinavyokaa vizuri kwenye nyama ndio inazidi kulainika na kuwa tamu, hivyo kuwa na subira.
 • Bandika kikaango (frying pan) jikoni. Weka mafuta kidogo sana. Acha yapate moto. Weka nyama kwenye mafuta. Acha nyama iive vizuri upande mmoja, kwa moto wa wastani. Usitoe hadi iive zivuri. Ikishaiva upande mmoja, geuza upande wa pili, acha iive.
 • Ukimaliza hifadhi pembeni, rudia kwa nyama zilizobaki.
 • Ukimaliza tenga viazi na nyama kwenye sahani. Jirambe kwa hamu yako.

1m


MAPISHI YAPENDWAYO

Mille feuille pastry
dakika 25
Walaji: 6

Sambusa za limao na asali
dakika 30
Walaji: 5

Vipopo
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.