Chips za kuoka zenye viungo

Unapenda chips lakini unaogopa mafuta mengi? Hapa umepata suluhisho. Hizi chips hazipikwi kwa kukaangwa na mafuta mengi, bali zinapikwa kwa kuokwa kwenye oven. Hizi chips ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma kutokana na viazi kuliwa vikiwa na maganda yake. Maganda ya viazi ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma. Cha zaidi, hivi viazi ni vitamu, vina ladha nzuri na vitakupa raha wakati wa kuvila. Jirambe.

Mahitaji

 • Viazi  mbatata 6
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Cayenne paper kijiko 1 kidogo
 • Chili sauce kijiko 1 kikubwa
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Mafuta ya kula vijiko 2 vikubwa
 • Bizari nyembamba
 • Kitunguu saumu 1, menya na ponda vizuri

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hizi chips ni tamu kutokana na uwepo wa viungo tofauti lakini pia ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma. Ni mapishi muafaka kwa wale wanaopenda kula chakula bora bila kutumia mafuta mengi. Kuwa huru kuongea au kupunguza viungo kulingana na upendavyo ladha yako ya chakula.

misosi-viazi-maganda-main

 • Osha viazi kwenye maji safi yasiyotuwama kisha kata vipande vyembamba vinavyofaa chips.

Usimenye maganda ya viazi. Maganda yana madini ya chuma, na yana faida kubwa ya kuboresha kiwango cha damu.

 • Weka viazi kwenye bakuli ya maji baridi na viache vilowe kwa takribani dakika 10.
 • Washa oven, weka kwenye nyuzijoto 375 °F(190°C).
 • Changanya pamoja mafuta ya kula, pilipili manga, cumin, chilli sauce, kitunguu saumu kilichopondwa, cayenne pepper, chumvi. Koroga vizuri hadi mchanganyiko uwe sawia.
 • Toa viazi kwenye bakuli la maji, acha vikauke. Hifadhi kwenye tissue paper (au paper towel). Changanya viazi kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa mafuta na viungo. Koroga vizuri hadi viazi vyote viendee vizuri.
 • Kwenye bakuli au sinia unalotumia kuoka kwenye oven (unaweza kuanza kuweka foil paper au kitu kisichonata ili kuzuia viazi visinati) weka viazi, hakikisha visipandiane. Kisha weka kwenye oven. Tega muda wa dakika 20. Muda ukiisha, geuza viazi na acha viive hadi vigeuke rangi na kuwa vigumu kiasi, itachukua kama dakika 20 nyingine.
 • Toa chips, andaa vizuri na ujirambe.

misosi-viazi-maganda


MAPISHI YAPENDWAYO

Biscuits za raspberry
dakika 15
Walaji: 5

Cornbread wenye zabibu kavu
dakika 40
Walaji: 3

Paella
dakika 30
Walaji: 8

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.