Chips zenye kamba, sweetcorn na mayai

Chakula hiki nimekifurahia maana kilikuwa kina ladha tofauti sababu ya kuwepo mchanganyio wa mahindi na kamba (prawns). Nimejaribu kula sweetcorn ikichanganywa na mayai pamoja na prawns. Ni mchanganyiko mmoja mzuri sana na unaweza pia kujaribu ili upate kujiramba zaidi na chakula hiki kitamu.

Mahitaji

 • Viazi 4
 • Mayai 2
 • Kamba (prawns) - tumia kiwango kinachokutosha
 • Chumvi
 • Karoti 1
 • Sweetcorn (Mahindi matamu)
 • Pilipili manga ya unga kijiko  1 cha chai
 • Limao 1 (au ndimu)
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Mafuta ya kupikia (nimetumia olive oil) – kadiria mafuta yanayotosha kupikia chips ulizoandaa.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Tunaandaa chakula kiki kwenye sehemu 3 tofauti. Mwisho tutakuwa na kitu kitamu kama hiki.

2msosimtamu

0. Andaa mahitaji

 • Menya karoti, kitunguu maji na kitunguu saumu. Kata kitunguu maji na karoti vipande vidogo, hifadhi vizuri pembeni. Ponda kitunguu saumu vizuri na hifadhi pembeni.
 • Andaa kamba (prawns) – toa maganda, osha vizuri. Weka kwenye chombo kisafi. Nyunyuzia chumvi kiasi. Mwagia limao au ndimu – hii inasaidia kuondoa shombo. Weka kitunguu saumu kwenye kamba. Nyunyuzia pilipili manga kiasi kwenye kamba. Koroga vizuri ili kamba wachanganyike na viungo. Acha kamba ili viungo viingie vizuri.
 • Andaa viazi – menya maganda. Osha kisha kata vipande vidogo vya chips. Hifadhi kwenye chombo chenye maji.

Mie huwa napenda kuweka chumvi kwenye viazi kabla sijaanza kupika, maana chumvi inaingia vizuri kabla sijapika, hivyo haina haja ya kuongeza chumvi wakati wa kula.

1. Andaa chips

 • Bandika kikaangio jikoni. Weka mafuta ya kula, acha yapate moto vizuri. Weka viazi na kuanza kukaanga hadi viive. Chips zikiiva hifadhi kwenye chombo pembeni. Usifunie ili zipate kuwa vizuri, maana ukifunika na mvuke wake zitalainika na kulowa maji.

Unaweza pia kuandaa chips kwa njia tofauti unayopendelea. Cha msingi upate chips ziliziva ili kula pamoja na vitu vingine.

2. Andaa kamba (prawns)

 • Bandika kikaango jikoni. Weka mafuta ya kula kidogo sana. Acha yapate moto. Weka kamba (prawns) kwenye mafuta. Acha waive kwa dakika 4 hadi 6 halafu weka karoti. Karoti zikilainika kidogo toa na weka kenywe sahani.

3. Andaa mayai

 • Pasua mayai kwenye chombo. Weka chumvi kisha koroga vizuri.
 • Bandika chungu jikoni, weka mafuta na kisha weka mahindi. Acha yapate kuiva kiasi, mwagia mayai, acha yapate kuiva vizuri pande zote mbili.
 • Tenga chakula na ujirambe.

msosimtamu

2msosimtamu


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi mshale za nazi
dakika 30
Walaji: 4

Cutlets za pilipili
dakika 5
Walaji: 4

Wali wenye nazi na maziwa
dakika 20
Walaji: 2

Nyama tamu yenye pilipili
dakika 25
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.