Chocolate crinkles

Mahitaji

 • Bitter sweet chocolate 225g
 • Icing sugar nusu kikombe
 • Sukari nyeupe vikombe 2
 • Butter vijiko 4 vya chakula
 • Mayai 4
 • Vanila kijiko kimoja na nusu cha chai
 • Unga vikombe 2
 • Baking powder kijiko 1 na nusu cha chai
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Espresso powder kijiko 1 (inatumika sana kwenye kubake vitu vya chocolate, huongeza ladha)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kwa kutumia mvuke, yeyusha chocolate na butter. Chukua sufuria bandika maji jikoni, yakichemka sana. 
 • Chukua sufuria nyingine weka chocolate na butter,chukua hiyo sufuria weka juu ya maji, mpaka viyeyuke.
 • Ikiyeyuka weka pembeni ipoe.
 • Pasua mayai yakoroge, weka sukari kwenye mayai koroga. Kisha weka vanila alafu chukua mchanganyiko wenye chocolate na butter changanya pia.
 • Hakikisha umechanganyika vizuri kisha weka pembeni.
 • Chukua bakuli lingine weka unga, baking powder, chumvi na espresso powder changanya vizuri.
 • Weka kwenye mchanganyiko ule wenye chocolate huku ukikoroga taratibu mpaka uchanganyike.
 • Funika mchanganyiko huo, weka kwenye fridge au uache masaa manne au uache usiku mzima mpaka uone umekua sio mgumu wala sio laini.
 • Weka icing sugar kwenye bakuli.
 • Chota mchanganyiko kwa kijiko au mikono, tengeneza mchunguko wa inch moja. Kisha zungusha kwenye bakuli la icing sugar. 
 • Hakikisha yote imeenea icing sugar. Hapo oven linakua na joto kidogo.
 • Weka chombo unachookea kipake butter au kuna karatasi waweza kutumia.
 • Ziweke kwenye oven kwa juu kabisa ili zipasuke ndani ya dakika 10 zitoe ziache zipoe, sasa jirambe

 


MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya pilipili
dakika 15
Walaji: 2

Chips mayai na mboga za majani
dakika 20
Walaji: 2

Mishikaki ya kupaka
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.