Chocolate Fondant Pudding

Chocolate fondant pudding ni kitindamlo (dessert) rahisi sana kinachoandaliwa kwa kutumia mayai, sukari, chocolate, siagi na unga wa ngano kiasi. Unaweza kuandaa hii pudding na kuhifadhi kwenye jokofu kwa kuila baadae. Muda unaotaka kula unaipasha moto kwa dakika chache na itakuwa safi kuliwa.

Mahitaji

 • Chocolate 200 g
 • Siagi (butter) 100 g
 • Sukari 100 g
 • Mayai 5
 • Unga wa ngano vijiko 4

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuandaa kwa kuongeza mahitaji unayopendelea zaidi.

misosi-chocolate-fondant-pudding-new

 • Bandika sufuria jikoni kwenye moto mdogo. Weka chocolate na siagi, acha hadi ziyeyuke vizuri.
 • Washa oven kwenye nyuzijoto 356°F (180 ° C), acha ipate moto vizuri.
 • Pasua mayai, tenganisha ute na viini. Hifadhi pembeni vizuri.
 • Mchanganyiko wa chocolate na siagi ukishayeyuka weka viini vya mayai, koroga pamoja vizuri. Weka sukari na unga, koroga vizuri pamoja. Weka ute wa yai kisha koroga vizuri zaidi hadi mchanganyiko uwe na ukungu wa mayai.
 • Paka vizuri chombo cha kuokea mafuta na unga. Mimina mchanganyiko wa chocolate na mayai kwenye chombo cha kuokea.
 • Weka chombo cha kuokea kwenye oven na tega dakika 20. Muda ukifika, toa chocolate pudding na hifadhi pembeni.
 • Ni vizuri kuila ikiwa ya moto ili kupata ladha zaidi. Unaweza kuipasha moto kwenye oven muda mchache kabla ya kuila kwenye moto wa wastani kwa dakika 5 hadi 10.

misosi-chocolate-fondant-pudding-main-poor


MAPISHI YAPENDWAYO

Supu ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.