Chocolate pancakes

Pancakes zinaweza kuliwa wakati wowote, kwa chakula cha asubuhi, mchana au jioni. Ni chakula kizuri pia kwa picnic, chakula cha watoto shule na pia chakula cha kwenda nacho ofisini.

Mahitaji

 • Unga wa ngano – kikombe 1½
 • Baking powder – vijiko 3 vidogo
 • Chumvi – kijiko 1 kidogo
 • Sukari – kijiko 1 kikubwa
 • Kikombe 1 cha maziwa
 • Yai 1
 • Vijiko 3 vya siagi (butter). Unaweza kutumia mafuta ya kula tofauti, kama hutumii siagi
 • Chocolate – ¼ kikombe

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Andaa hizi pancakes kupata chakula rahisi jioni. Hakikisha unatumia mafuta utakayopenda kama hutumii siagi.

misosi-pancakes-main1

 • Chekecha unga kwenye bakuli kubwa. Weka baking powder, chumvi na sukari, changanya vizuri kisha tengeneza shimo katikati ya unga. Weka maziwa, pasua yai na butter iliyoyeyushwa. Changanya vizuri kwa pamoja hadi mchanganyiko uwe laini.
 • Weka kikaangio jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka siagi ya kutosha kwenye kikaango, kisha weka mchanganyiko wa unga kwa kutumia upawa au chombo kinachofaa. Pika upande mmoja hadi ubadilike rangi na kuanza kuwa na rangi ya udongo (brown).
 • Ukishatoa jikoni, tandaza chocolate juu yake. Kula zikiwa za moto kwa ladha nzuri zaidi.
 • Nyama ya kusaga ilipikwa kwa kukaangwa kawaida, bila mafuta, kwa moto wa wastani. Kama ilivyoelezwa hapa.

misosi-pancakes-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Chachandu ya embe
dakika 15
Walaji: 4

Bagia za kunde
dakika 7
Walaji: 4

Maandazi ya Vanila na Nazi
saa 1
Walaji: 15

Pound cake
dakika 60
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.