Cookies za limao na mayai

Tunatumia sana limao kama kiungo cha chakula kwa kuboresha ladha , leo basi tunatumia kwa kuweka ladha zaidi kwenye vitafunwa vya limao vyenye mayai ili kunogesha ladha. Ni vitafunio vizuri kupika kwa kupata chai au kahawa.

Mahitaji

 • Unga wa keki wenye ladha ya limao ½ kilo
 • Mayai 2, pasua kisha koroga vizuri
 • Mafuta ya kula robo tatu ya kikombe
 • Maji ya limao kijiko 1 cha chai
 • Icing sugar robo tatu ya kikombe
 • Lemon zest kijiko 1 cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Washa oven, weka nyuzijoto 375°F (190°C)
 • Kwenye bakuli kubwa – weka unga, mayai, mafuta ya kula, maji ya limao na lemon zest. Changanya hadi unga uchanganyike vizuri na vitu vingine. Ukiona unga unanata sana mikononi, hifadhi kwenye jokofu (fridge) kwa dadika 10. Hii itasaidia kuufanya unga uache kunata.
 • Weka sukari kwenye bakuli. Kwa kutumia unga ulichonganywa, tengeneza umbo la cookies unalopendelea kisha ziweke kwenye bakuli ya sukari. Hakikisha pande zote za cookie zimeenea sukari (icing sugar). Rudia hii hadi umalize unga wote kutengeneza cookies.
 • Weka kwenye oven, oka kwa muda wa dakika 10 mpaka 15 kisha toa.
 • Acha zipoe kisha jirambe.

misosi-lemon-cookies-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Salad yenye sausage
dakika 5
Walaji: 1

Supu ya Kuku
dakika 30
Walaji: 4

Sandwich ya kienyeji
dakika 7
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.