Cornbread wenye zabibu kavu

Cornbread, mkate wenye ladha tamu, harufu nzuri na ubora wa kuliwa wakati wowote ule. Ni mkate wenye mchanganyiko wa ngano na unga wa mahindi. Mapishi haya yanajumuisha maziwa, butter na asali, ambayo huufanya mkate kuwa mtamu na wenye harufu ya kuvutia zaidi. Ni pishi unaloweza kuandaa ili kuipa familia yako ladha zaidi.

Mahitaji

 • Sukari nyeupe kikombe 1
 • Unga wa mahindi kikombe 1½
 • Ngano ½ kikombe
 • Baking soda ½ kijiko cha chai
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Butter ½ kikombe
 • Butter ¾ kikombe
 • Asali vijiko 3 vya chai
 • Maziwa kikombe 1¼
 • Zabibu kavu ½ kikombe
 • Mayai 4

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Bandika sufuria jikoni, weka butter (¾ kikombe), acha iyeyuke. Epua kisha weka sukari na mayai kwenye sufuria. Koroga pamoja hadi vilainike vizuri. Changanya baking soda na maziwa kisha weka kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa mayai.
 • Koroga pamoja vizuri.
 • Weka unga wa mahindi, unga wa ngano na chumvi kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa mayai. Changanya vizuri mpaka mabonge yapotee na mchanganyiko uwe laini wastani (siyo mzito wala mwepesi).
 • Weka asali na zabibu kavu kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa unga. Changanya vizuri kisha
 • Weka mchanganyiko kwenye chombo unachotumia kuokea. Hayo maua kwenye mkate yapo kwenye hicho chombo. Tega muda kati ya dakika 30 hadi 40. Hapo mkate utakua tayari.
 • Epua mkate kisha paka vizuri ½ kikombe cha siagi juu ya mkate ili kuupa ladha tamu zaidi. Acha upoe kisha jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Mtori wa ndizi
dakika 45
Walaji: 1

Pilipili ya maembe ya kusaga
dakika 35
Walaji: 5

Chicken with mashed potato
dakika 30
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.