Cornbread yenye korosho

Cornbread, mkate wenye ladha tamu, harufu nzuri na ubora wa kuliwa wakati wowote ule. Ni mkate wenye mchanganyiko wa ngano na unga wa mahindi. Mapishi haya yanajumuisha maziwa, butter na asali, ambayo huufanya mkate kuwa mtamu na wenye harufu ya kuvutia zaidi. Ni pishi unaloweza kuandaa ili kuipa familia yako ladha zaidi.

Mahitaji

 • Sukari nyeupe  kikombe 1
 • Unga wa mahindi kikombe 1½
 • Ngano ½ kikombe
 • Baking soda ½ kijiko cha chai
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Butter ½ kikombe
 • Butter ¾ kikombe
 • Asali vijiko 3 vya chai
 • Maziwa kikombe 1¼
 • Korosho au zabibu kavu ½ kikombe

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mkate huu wenye ubora wa kipekee umeandaliwa na Jesse Biseko. Picha na maelezo ya mapishi haya kwa idhini na  ruksa ya na Jesse Biseko. Asante kwa kutushirikisha kujifunza kitu kipya.  

msosi-cornbread

 • Pasha oven nyuzi joto 350°F (180°C). Paka mafuta vizuri ndani ya chombo unachotumia kuokea mkate.

misosi_cornbread_01

 • Bandika sufuria jikoni, weka butter (¾ kikombe), acha iyeyuke. Epua kisha weka sukari na mayai kwenye sufuria. Koroga pamoja hadi vilainike vizuri. Changanya baking soda na maziwa kisha weka kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa mayai. Koroga pamoja vizuri.
 • Weka unga wa mahindi, unga wa ngano na chumvi kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa mayai. Changanya vizuri mpaka mabonge yapotee na mchanganyiko uwe laini wastani (siyo mzito wala mwepesi).
 • Weka asali na korosha kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa unga. Changanya vizuri kisha.

misosi_cornbread_11

 • Weka mchanganyiko kwenye chombo unachotumia kuokea. Tega muda kati ya dakika 30 hadi 40. Hapo mkate utakua tayari.

misosi_cornbread_1

misosi_cornbread_2

 • Epua mkate kisha paka vizuri ½ kikombe cha siagi juu ya mkate ili kuupa ladha tamu zaidi. Acha upoe kisha jirambe.

misosi_cornbread_main

misosi_cornbread_3


MAPISHI YAPENDWAYO

Couscous
dakika 100
Walaji: 4

Chips na kuku
dakika 45
Walaji: 3

Spice potato curry
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.