Couscous

Couscous (inatamkwa kus kus) ni chakula chenye asili ya afrika kaskazini, hasa kwenye nchi za kiarabu za sahara – Morocco, Algeria na nyingine. Ni chakula kinachopikwa kwa kutumia mvuke, chenye utamu wa kipekee na kinachoweza kupikwa kwa kuongeza viungo tofauti, kama ilivyo wali. Couscous inapatikana kwenye maduka yanayouza vyakula asili ya kiarabu na kihindi, pia unaweza kupata kwenye supermarket tofauti.

Mahitaji

 • Couscous – ½ kilo (couscous inapatikana supermarket au maduka ya vyakula asili ya kiarabu na kihindi)
 • Maji 
 • Viazi  mbatata 2
 • Karoti 1
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu saumu cha unga
 • Parsley
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya ya couscous (inatamkwa kus kus) ni rahisi na hayahitaji vitu vingi sana ili kupikwa. Unachotakiwa ni kuwa na jiko linaloweza kupika kwa mvuke au unaweza kutumia couscoussier, jiko maalum la kupikia couscous. Kwenye mapishi haya nimetumia rice cooker na chakula kimetoka vizuri.

misosi-couscous-main

 • Kata karoti, pilipili hoho kwenye vipande vikubwa, maana vitakaa kwenye maji muda mrefu. Weka kwenye sufuria ya rice cooker. Menya viazi, osha kisha weka kwenye sufuria ya rice cooker, usivikate. Weka parsley kwenye sufuria ya rice cooker. Ongeza maji kwenye sufuria ya rice cooker hadi yazidi nusu ya sufuria kisha weka jikoni acha hadi ianze kuchemka.
 • Kwenye sufuria tofauti, changanya maji lita 1,chumvi na kitunguu saumu cha unga. Weka jikoni, acha yachemke vizuri na yachanganyike vizuri.
 • Weka couscous kwenye bakuli kubwa, mwagia maji yenye chumvi na kitunguu saumu, yawe ya uvuguvugu. Anza kuchanganya taratibu kwa mikono ili couscous inyonye maji vizuri. Changanya hadi maji yapotee kisha weka couscous kwenye sufuria yenye matundu kwa chini, mara nyingi huwa pamoja na rice cooker. Tandaza couscous vizuri bila kuikandamiza. Weka sufuria juu ya sufuria ya rice cooker inayochemka. Acha ichemke pamoja kwa dakika 60.
 • Baada ya dakika 60, au saa 1, toa couscous, mimina kwenye bakuli kubwa, koroga vizuri. Hakikisha punje zinabaki mojamoja, kama kuna mabonge yamejijenga, mungunyua ili zibaki punje ndogo. Rudishia couscous kwenye sufuria yenye matundu kwa chini. Ongeza maji kwenye sufuria ya rice cooker, hakikisha yawe nusu kama ilivyokuwa mwanzo. Kisha weka sufuria yenye couscous juu yake.  Acha ichemke kwa dakika nyingine 20. Unaweza kuongeza viungo unavyopenda kwenye maji yaliyomo kwenye sufuria ya rice cooker ili kuipa couscous harufu nzuri.
 • Baada ya dakika 20, toa couscous, chambua ili zibaki chembe ndogondogo, kisha rudishia kwenye sufuria, weka juu ya sufuria ya rice cooker jikoni. Hakikisha maji yako mengi.  Acha maji yachemke kwa dakika nyingine 20. Kisha rudia hatua hii – toa, chambua na urudishie jikoni kwa dakika nyingine 20.
 • Toa couscous, andaa kwenye sahani. Weka viambato vilivyo kwenye sufuria ya rice cooker, kisha jirambe kwa ladha yako.
 • Kwenye chakula hiki nilitumia samaki wa kukaanga, sauce ya bilinganya na spinach ambazo nilipika tofauti. Nilipenda uwepo wake kwenye chakula.

misosi-couscous-main0


MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa kuku na mayai yake
dakika 40
Walaji: 4

Viazi vya mboga mboga
dakika 18
Walaji: 2

Salad ya mahindi na samaki
dakika 0
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.