Cream cheese pound cake

Hii ni keki rahisi sana kuandaa yenye kukupa matokeo mazuri. Uwepo wa vanilla huifanya keki hii kuwa na harufu ya kuvutia. Vilevile kuna viungo kama zabibu, cream cheese, sukari na siagi.

Mahitaji

 • Unga wa ngano vikombe 3
 • Sukari nyeupe vikombe 2
 • Vanilla kijiko 1 cha chai
 • Cream cheese ¼ kilo
 • Siagi (Butter) ¼ kilo
 • Baking powder kijiko 1 cha chai
 • Mayai 6
 • Zabibu kavu kiasi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza au kupunguza mahitaji kutokana na unavyopendelea.

 • Pasha oven nyuzijoto 325°F (165°C). Paka mafuta na nyunyizia unga kiasi kwenye chombo cha kuokea.
 • Kwenye bakuli kubwa changanya siagi (butter) na cream cheese changanya mpaka ichanganyikane vizuri. Kisha ongeza sukari kwa awamu huku ukichanganya mpaka ilainike vizuri.
 • Pasua mayai kwa awamu - mawili kila wakati – huku ukikoroga vizuri kila unapoweka mayai. Ukimaliza kuweka mayai, weka unga na changanya vizuri hadi mchanganyiko uwe sawia na mchanganyiko wa mayai vizuri. Weka vanilla, changanya pamoja na unga.
 • Panga zabibu kavu kwenye chombo cha kuokea. Mimina mchanganyiko wa keki kwenye chombo cha kuokea na oka kwa muda wa saa 1 na dakika 20.
 • Muda ukifika, chomeka kisu au chochote chenye ncha kali (mfano toothpick). Kikitoka kikavu keki itakuwa imeshaiva vizuri. Acha keki ipoe kwa muda kabla ya kujiramba.

misosi-pound-cake-poor


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi mzuzu na sausage
dakika 10
Walaji: 1

Salad ya samaki
dakika 15
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.