Creamy rice pudding

Rice pudding ni chakula kizuri na kitamu sana. Chakula hiki anaweza kula mtoto na mtu mzima

Mahitaji

 • Mchele mweupe Kikombe 1
 • Maziwa vikombe 2
 • Sukari nyeupe nusu kikombe
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Yai 1
 • Apple 1
 • Butter kijiko 1 cha chakula
 • Vanilla nusu kijiko cha chai
 • Nutmeg kiasi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Osha mchele, bandika maji vikombe 2 jikoni. Yakichemka weka mchele kisha punguza moto. Funika acha ichemke kwa dakika 20.
 • Sufuria jingine weka mchele uliopikwa, maziwa kikombe 1 na nusu, sukari na chumvi.
 • Funika punguza moto, pika kwa dakika 20.
 • Ongeza maziwa nusu kikombe, yai na apple. Pika kwa dakika 2 koroga bila kuacha. Epua.
 • Weka butter, nyunyia nutmeg na vanilla. Acha kipoe kidogo mpe mtoto ale. Mi leo nimemsagia.

MAPISHI YAPENDWAYO

Chips na kuku
dakika 45
Walaji: 3

Spice potato curry
dakika 30
Walaji: 4

Spinach yenye maziwa na nazi
dakika 5
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.