Cutlets za nyama au samaki

Cutlets inatakiwa kupikwa na nyama laini inayoiva haraka. Hizi cutlets unaweza kuzila kwa wali au chakula kingine; unaweza pika kutafuna kwa hamu mdomoni kama wajisikia haja ya kula kitu kitamu.

Mahitaji

 • Viazi ulaya ½ kilo
 • Chumvi
 • Pilipili mbuzi 1
 • Vitunguu saumu 2
 • Vitunguu maji 2
 • Karoti 2
 • Nyama (unaweza pia kutumia samaki) ½ kilo
 • Unga wa ngano ( unaweza pia kutumia sembe) ¼ kilo
 • Mayai 2

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa nyama – osha na kata vipande vidogo.
 • Andaa viungo – osha na kata vitunguu saumu na vitunguu maji na karoti – kata kwenye vipande vidogo. Ponda vitunguu saumu.
 • Weka viungo kwenye nyama – weka kitunguu saumu na chumvi.
 • Chemsha nyama. Unaweza kuchemsha na pilipili ili kuipa harufu na ladha nzuri. Chemsha hadi maji yakauke kwenye nyama. Kama unatumia samaki utafanya vivyo hivyo.
 • Changanya nyama na viazi – unaweza pia kuweka nyama kati ya viazi. Kama unatumia samaki, unaweza kusaga samaki na kuchanganya na viazi ili kupata mchanganyiko sawia wa wa samaki na viazi.
 • Gonga mayai 2 na koroga vizuri.
 • Chukua kiazi chenye nyama (au samaki) chovya kwenye mayai halafu nyunyuzia unga (au sembe) au unaweza kuchovya pia.
 • Weka kwenye mafuta jikoni ili kukaanga.
 • Vikiiva vizuri toa na weka pembeni. Jirambe

MAPISHI YAPENDWAYO

Roast ya kuku, nazi na maziwa
dakika 25
Walaji: 2

Wali wa nazi na maziwa
dakika 10
Walaji: 2

Mapishi ya tambi na kamba
dakika 20
Walaji: 2

Maandazi ya Mayai na Maziwa
dakika 20
Walaji: 4

Toa maoni yakoolivia adam
09:22, Sat 01 Nov 2014
Habari misosi mitamu leo nimejaribu kupika cutles za nyama ziko poa sana na jana rosti ya maini it full kujiramba kwenye family yangu
Dadia Msindai
13:36, Mon 03 Nov 2014
@Olivia Adam, karibu sana na tunashukuru kwa feedback yako. Tunafurahi kama umejiramba kwa mapishi matamu. Karibu sana uendelee kupata vionjo vitamu zaidi vya misosi.

Endelea kujiramba na familia kwa chakula bora zaidi.
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.