Dagaa wa kuunga na nazi

Dagaa, chanzo cha madini ya chuma mwilini. Ni chakula bora kwetu sote – wakubwa na watoto. Mapishi haya ya dagaa kwa nazi yanakupa ladha tofauti ya kukufanya kujiramba zaidi na kuongeza hamu ya kula kwako na wale uwapendao

Mahitaji

 • Dagaa ½ kilo
 • Vitunguu vikubwa 2
 • Nyanya 4
 • Pilipili hoho 1
 • Karoti 1
 • Nazi 1
 • Vitunguu swaumu 1
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Mafuta ya kula
 • Ndimu 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Anza kuandaa dagaa – kata vichwa, toa matumbo, osha na kisha weka vizuri kwenye sufuria.
 • Andaa kitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti. Osha, kata vipande vidogo tayari kwa mapishi.
 • Andaa tui la nazi – vunja nazi, kuna na kisha kamua tui zito na hifadhi vizuri pembeni.
 • Weka sufuria ya kupikia jikoni, kisha mimina mafuta ya kula kiasi. Subiria yapate moto vizuri.
 • Weka vitunguu kwenye sufuria. Koroga ili kufanya viive vizuri.
 • Kabla vitunguu havijaiva vizuri, weka dagaa. Koroga na kukaanga vizuri dagaa.
 • Dagaa wakianza kukauka kamulia ndimu juu yake. Koroga kiasi kisha weka pilipili hoho na karoti. Endelea kukoroga.
 • Weka nyanya kwenye dagaa. Endelea kukoroga na kisha funika na mfuniko ili nyanya ziive vizuri na mvuke na kuwa laini.
 • Nyanya zikiiva unaweza kuziponda ili kupata rojo nzuri.
 • Weka chumvi unayoona inafaa kutokana na kiwango cha mboga.
 • Ongeza tui zito la nazi, endelea kukoroga ili tui lisikatike. Acha tui lichemke hadi liishe na ubaki mchuzi mzito.
 • Unaweza kuepua dagaa wako na kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Wali & mboga mseto
dakika 45
Walaji: 4

Pilau la basmati
dakika 35
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.