Dagaa wa nazi na karanga

Iwe unapenda au hupendi dagaa, hii mboga lazima ikupe hamu ya kula chakula, hasa ugali ulio na pilipili. Kwanza muonekano wake unavutia, mbili karanga zinaleta ladha yake wakati tui la nazi linaipa harufu ya kipekee. Siwezi kuelezea utamu wake, hii ni mboga ya kuonja tu, hakuna kingine.

Mahitaji

 • Dagaa gramu 100 (Angalia kipimo kinachotosha)
 • Pilipili hoho 2
 • Peanut butter vijiko 2 vikubwa
 • Limao 1
 • Chumvi
 • Mafuta ya kula
 • Bamia 6, kata ncha, kata vipande vidogo vidogo
 • Nyanya maji za wastani 3 au unaweza kutumia tomato paste
 • Nyanya chungu 2 – chemsha kwa dakika 5, toa Maganda na hifadhi pembeni
 • Tui zito la maji - 1/2 kikombe

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Nilikuwa nataka kujaribu mchanganyiko wa karanga na nazi kwenye dagaa. Matokeo yake yakawa si mchezo, maana dagaa hawa wana kila aina ya kionjo unachotaka kukipata kwenye chakula. Rojo la daa zito linalofaa kuliwa na vyakula vingi tofauti. Uwepo wa mboga za majani hukifanya huwapa dagaa utamu zaidi. Nilifurahi wakati wa kula, maana ni chakula kitamu na chenye afya.

misosi-dagaa-main2

 • Andaa dagaa – kata vichwa, toa uchafu. Osha kisha weka pembeni. Andaa kitunguu maji – menya kisha kata vipande vidogo. Kata pilipili hoho kwenye vipande vidogo. Hifadhi pembeni.
 • Chemsha nyanya chungu kwenye sufuria yenye maji kiasi. Nyanya chunu zikiivia, menya ngozi ya juu na hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria au kikaango jikoni, weka mafuta ya kula kiasi. Yakichemka weka kitunguu saumu, koroga. Weka kitunguu maji. Koroga, acha viive na kulainikia kiasi – takribani dakika 3. Ongeza chumvi kiasi. Weka dagaa, kwenye sufuria. Koroga vizuri. Funika vizuri. Acha dagaa wakaangike kiasi kwenye mafuta.
 • Ongeza nyanya, koroga kiasi kisha funika acha ziive vizuri.

Kama ni fresh tomato unaweza kuziponda ili zilainike na kuwa uji baada ya muda, kama ni tomato paste acha ziive tu. Hakikisha hazikauki na kuungua tu, unaweza kuongeza maji kiasi au supu ya nyama ili ziendelee kuiva vizuri.

 • Baada ya dakika kama 8 hadi 10 baada ya nyanya kuchemka, ongeza pilipili hoho na karoti. Koroga vizuri kisha funika.

Mie huwa napenda pilipili hoho zisiive sana, ili nipate virutubisho zaidi na pia harufu nzuri ya pilipili hoho. Kama unapenda ziive vizuri unaweza kuweka mapema ili zikae jikoni muda mrefu, lakini unapunguza virutubisho kwa kuziweka muda mrefu kwenye moto.

 • Sauce ya nyanya ikishaiva weka nyanya chungu. Koroga pamoja vizuri. Kamulia limao, unaweza kuweka nusu ili mboga isiwe chachu sana. Koroga vizuri. Acha ichemke kwa dakika 2 hadi 3.
 • Weka vijiko 2 vya peanut butter. Ukiona mchuzi mzito sana, ongeza maji kiasi kabla ya kuweka tui la nazi. Kisha koroga na acha lichemke kwa dakika 2.
 • Weka tui la nazi kwenye dagaa. Koroga hadi tui lianze kuchemka, kisha funika kwa dakika 5 ili tui na karanga vichanganyike na dagaa. Acha ichemke kwa dakika 3 hadi 5 kisha epua.
 • Hii mboga inaweza kuliwa pamoja na vitu vingine mfano mkate, chapati, maandazi, au hata wali na ugali. Ni chaguo lako. Binafsi niliweza kula mboga tu baada ya kuonja na kuona utamu wake.

misosi-dagaa-main

misosi-dagaa-final


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.