Dagaa wenye curry sauce

Kuna aina tofauti za kupika dagaa. Mie napenda kuongeza vionjo tofauti ili kuwafanya dagaa wavutie zaidi. Kwenye mapishi haya nimetumia curry powder ili kuwapa dagaa ladha na harufu tamu. Ni mboga nzuri inayoweza kuliwa na chakula chochote. Pia dagaa hawa wana bamia, pilipili za kijani, kitunguu saumu, nyanya na limao.

Mahitaji

 • Dagaa ¼ kilo
 • Pilipili hoho 2
 • Bamia 4, kata ncha, kata vipande vidogo vidogo
 • Curry powder vijiko 2 vikubwa
 • Limao 1
 • Chumvi
 • Pilipili za kijani, kata vipande vidogo vidogo
 • Kitunguu saumu punje 3, menya na saga. Unaweza pia kutumia cha unga.
 • Nyanya maji za wastani 3 au unaweza kutumia tomato paste

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza mahitaji kulingana na unavyopendelea.

 • Andaa dagaa – toa uchafu, unaweza kukata vichwa kama unapendelea. Osha kisha weka pembeni. Andaa kitunguu maji – menya kisha kata vipande vidogo. Kata pilipili hoho kwenye vipande vidogo. Hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria au kikaango jikoni, weka mafuta ya kula kiasi. Yakichemka weka kitunguu saumu, koroga. Weka kitunguu maji. Koroga, acha viive na kulainikia kiasi – takribani dakika 3. Ongeza chumvi kiasi. Weka dagaa kwenye sufuria. Koroga vizuri kisha funika na acha dagaa wakaangike kiasi kwenye mafuta.
 • Ongeza nyanya, koroga pamoja vichanganyike kisha funika acha ziive vizuri. Kama ni fresh tomato unaweza kusubiria dakika chache ziive na uziponde ili zilainike na kuwa uji baada ya muda, kama ni tomato paste acha ziive tu. Hakikisha hazikauki na kuungua tu, unaweza kuongeza maji kiasi au supu ya nyama ili ziendelee kuiva vizuri.
 • Baada ya dakika kama 8 hadi 10 baada ya nyanya kuchemka, ongeza pilipili hoho, karoti na pilipili za kijani. Koroga vizuri kisha funika.
 • Mie huwa napenda pilipili hoho zisiive sana, ili nipate virutubisho zaidi na pia harufu nzuri ya pilipili hoho. Kama unapenda ziive vizuri unaweza kuweka mapema ili zikae jikoni muda mrefu, lakini unapunguza virutubisho kwa kuziweka muda mrefu kwenye moto.
 • Sauce ya nyanya ikishaiva weka curry powder. Koroga pamoja vizuri. Kamulia limao, unaweza kuweka nusu ili mboga isiwe chachu sana. Koroga vizuri. Acha ichemke kwa dakika 5 hadi 7.
 • Hii mboga inaweza kuliwa pamoja na vitu vingine mfano ugali, chapati, maandazi, wali au mkate. Ni chaguo lako, jirambe na utamu wa hii mboga ya dagaa wa curry sauce.

misosi-dagaa-curry-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wa kukaanga
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.