Dessert ya matunda – strawberry, apple na ndizi

Napenda kula mlo mkuu huku nikikamilisha na kitindamlo kama hiki. Ni kiambato kinachoweza kukufanya upumzike dakika chache huku ubongo wako ukipata utamu na uhondo wa sukari kwa ajili ya ubongo wako kufanya kazi vizuri.

Mahitaji

 • Apple
 • Strawberries
 • Maziwa (Maziwa fresh au mtindi)
 • Sukari
 • Ndizi za kuiva
 • Vanilla

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuandaa dessert hii kwa kutumia tunda moja, hasa strawberry, au unaweza kuchanganya matunda tofauti ili kupata ladha na virutubisho zaidi.

 • Andaa matunda kwa kuosha na kisha kuyakata vizuri.
 • Kata strawberry vizuri na weka kwenye bakuli (au chombo unachotengenezea dessert yako)
 • Kata ndizi kwenye vipande vidogo na uchanganye kwenye strawberry.
 • Menya na kisha kata apple kwenye vipande vidogo, changanya pia kwenye matunda mengine.
 • Kwenye bakuli tofauti, weka maziwa kiasi, changanya sukari na kisha koroga ili sukari ipate kuyeyuka. Hakikisha maziwa ni ya baridi, maana hiki ni kinywaji baridi
 • Weka matunda kwenye maziwa, koroga kiasi. Ongeza Vanilla ili kuipa ladha na harufu tamu dessert yako.
 • Unaweza kuacha mchanganyiko kwa muda mfupi kwenye jokofu, au unaweza kula moja kwa moja.
 • Unaweza pia kuchanganya parachichi au nanasi kwenye mchanganyiko ili kuongeza utamu.
 • Jirambe na maisha.

MAPISHI YAPENDWAYO

Couscous
dakika 100
Walaji: 4

Chips na kuku
dakika 45
Walaji: 3

Spice potato curry
dakika 30
Walaji: 4

Spinach yenye maziwa na nazi
dakika 5
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.